Patanisho: Jamaa aachwa na mkewe mjamzito baada ya kumpiga, ajuta na kumlilia arudi

"Alisema hawezi kurudi. Hakunipa sababu," Kevin alisema.

Muhtasari

•Kevin alisema mkewe ambaye ni mjamzito aliondoka bila ilani wakati akiwa kazini baada ya kumpiga kufuatia mzozo wa kinyumbani.

•Jaribio la kuwapanisha wawili hao hata hivyo liligonga mwamba kwani Lydia hakushika simu wakati Gidi alipompiga.

Image: RADIO JAMBO

Kevin Moreka Nyangau ,26, kutoka Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Lydia Kemunto ,21, ambaye alikosana naye miezi miwili  iliyopita.

Kevin alisema mkewe ambaye ni mjamzito aliondoka bila ilani wakati akiwa kazini baada ya kumpiga kufuatia mzozo wa kinyumbani.

"Nilikuwa na simu. Ilikuwa imeharibika. Yeye ndo alikuwa ameharibu. Nikaamua niuze ninunue ingine. Hiyo ndo ilileta shida. Nilipomwambia nimeuza alianza kunitusi. Nilikasirika nikampiga kofi. Baada ya kumpiga niliomba msamaha. Nilitoka nikaenda shughuli zangu. Kumbe alikuwa amepanga kuenda," Kevin alisimulia.

Aliendelea, "Nimejaribu kuongea na yeye akasema nimtumie nauli arudi. Baadaye alikasirika akasema nisitume hatarudi. Tulikuwa tumeogea Ijumaa, alisema nitume Jumamosi ndio arudi Jumapili ama Jumatatu. Jioni alibadilisha wazo akasema nisitume hatarudi. Huwa naongea na mama yake. Alisema hajamuona nyumbani. Ako kwa dadake."

Kevin alisema ilikuwa mara ya kwanza kumpiga mkewe.

"Alisema hawezi kurudi. Hakunipa sababu," Kevin alisema.

Jaribio la kuwapanisha wawili hao hata hivyo liligonga mwamba kwani Lydia hakushika simu wakati Gidi alipompiga.

Kevin alipopewa nafasi ya kuzungumza na mkewe hewani alisema, "Babe najua nilikosea. Ningetaka kujua mahali ulienda. Bado nakupenda. Ningependa urudi."

Je, una ushauri gani kwa Kevin?