Patanisho: Jamaa aachwa kwa kumdangaya mkewe hatumii mihadarati ilhali anatumia sigara, muguka, pombe

"Bado nakupenda sana. Nataka urudi nyumbani tuendelee na maisha yetu," Titus alimwambia Linet.

Muhtasari

•Titus alisema kuwa ndoa yake ya mwaka mmoja ilisambaratika mwaka wa 2021 wakati mkewe alipogundua anatumia mihadarati. 

•"Sijui alijua aje natumia mihadarati. Sigara Nilianza kuvuta nikiwa darasa la nne," Titus alisema.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Titus Mutinda ,26, kutoka Machakos alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Linet Mutua ,24, ambaye alikosana naye takriban miaka miwili iliyopita.

Titus alisema kuwa ndoa yake ya mwaka mmoja ilisambaratika mwaka wa 2021 wakati mkewe alipogundua anatumia mihadarati. Alisema awali alikuwa amemdanganya Linet kuwa hatumii mihadarati ilhali alikuwa akitumia sigara, muguka na pombe.

"Alikuwa bibi yangu. Tulioana 2020. Wakati huo nilikuwa nafanya bodaboda, ikawa kazi haifanyi vizuri. Aliuliza kama natumia mihadarati nikamwambia situmii. Hata hivyo nilikuwa navuta sigara, nakula muguka na nakunywa pombe. Sijui alijua aje. Tulikuwa tunakaa na yeye lakini wakati mwingi alikuwa anakaa kwao. Ilifika wakati ikawa simu yangu hashiki, wakati nikituma meseji hajibu," Akothee alisema.

Titus alisema ilifika mahali akahama kutoka Kitengela na kuenda Kitui na kuwa mbali na mpenzi huyo wake.

"Nikipiga simu ashike tunaweza ongea vizuri. Lakini baada ya hapo mambo yanabadilika. Sijui alijua aje natumia mihadarati. Sigara nilianza kuvuta nikiwa darasa la nne. Ikafika mahali nikaacha kwa muda. Nilikuwa navuta mara moja moja. Vile nilimaliza shule ndio mihadarati iliniingia. Niliacha mihadarati mwaka jana nikiwa Kitengela. Sijatumia chochote kwa muda. Nilikuwa natumia sigara ya kawaida," alisema.

Aliongeza, "Wakati mwingine huwa tunakutana tu.Tukikutana hawezi kupita. Huwa tunaongea ni kama hatujawahi kukosana. Huwa tunazungumza vile atarudi lakini baada ya hapo hatarudi. Mama yake anaweza kushika akisikia ni mimi anakata. Yeye aliniambia hana mtu. Vile nilipatana na yeye ndio tulikuwa tumekosana na ex wangu. Tulikosana tu kwa mambo ya simu. Aliniambia mambo yangu hataki. Tuliachana kabisa. Aliniambia ashamove on.".

Kwa bahati mbaya, Titus hakuweza kupatanishwa na Linet kwani alipopigiwa simu mara kadhaa hakushika.

Wakati Titus alipopewa nafasi ya kuzungumza naye hewani, alimwambia, "Bado nakupenda sana. Nataka urudi nyumbani tuendelee na maisha yetu. Ni hayo tu."

Je, ushauri wako kwa Titus ni upi?