“Hii imeenda!” Jamaa ahuzunika baada ya mpenziwe kumruka, kumkataa na kumuita ‘dramatic’

Moreen alidai kwamba Karanja hadi aliwahi kumripoti katika kituo cha polisi baada ya wao kukosana.

Muhtasari

•Karanja alisema uhusiano wao wa mwaka mmoja ulivurugika mwezi Julai wakati alipomfumania mpenziwe na jamaa mwingine.

•Moreen alipopigiwa simu, alidai kwamba Karanja ana vituko sana na kubainisha kuwa hataki mahusiano naye tena.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Jamaa kwa jina David Karanja kutoka Lanet, Nakuru mwenye umri wa miaka 25 alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Moreen Atieno (21) ambaye alikosana naye takriban miezi mitatu iliyopita.

Karanja alisema uhusiano wao wa mwaka mmoja ulivurugika mwezi Julai wakati alipomfumania mpenziwe na jamaa mwingine.

"Tulikuwa tumekaa na yeye mwakam moja.Tulikuwa katika harakati ya kupanga hatua nyingine. Nilipata kazi mbali ambayo ilifanya tukose kuonana, akaanza kubadilika kwa umbali. Nilifuatilia, nikasafiri hadi Nakuru nikampata na mpango wa kando. Niliwapata pamoja nikamuuliza ni nini inaendelea. Kutoka hiyo siku hatuelewani," Karanja alisimulia.

Aliongeza, "Kwa sasa sijui kama ananitambua kama mumewe. Mimi niko mbali. Mawasiliano sio mazuri, akishika simu anakata. Nimeongea hadi na wazazi wake wakaniambia wataongea na yeye lakini bado imeshindikana."

Karanja alibainisha kwamba ingawa walikuwa wamechumbiana kwa mwaka mmoja, bado hawakuwa wamepata mtoto.

Moreen alipopigiwa simu, alidai kwamba Karanja ana vituko sana na kubainisha kuwa hataki mahusiano naye tena.

"Nilimwambia kuwa sitaki maneno yake. Yeye ni so dramatic, ana maneno mengi. Ako na vituko. Ameniaibisha tu. Kwanza, amedanganya jina langu. Naitwa Moreen, jina la pili amewadanganya Maneno ya mahusiano na kuoana pia ni uongo. Hatukuwa tumepanga kuoana na yeye, ilikuwa tu maneno ya boyfriend na girlfriend. Hatukuwa tumeoana na yeye. Ilikuwa boyfriend, girlfriend na iliisha. Hata mamangu anajua simtaki," Moreen alisema.

Moreen alidai kwamba Karanja hadi aliwahi kumripoti katika kituo cha polisi baada ya wao kukosana.

"Ako dramatic sana, kukosana kidogo, ashaambia mamangu mambo ya uongo. Hataki tukae chini kama watu wazima. Mtu anakupeleka hadi police station, huyo ni mtu tunaweza kuoana kweli. Ameniaibisha sana. Mwambie sitaki maneno yake," alisema.

Aliongeza, "Hakuna wazazi wangu anajua. Ni ile tu alipata namba ya mamangu kighafla. Badala apatie mama yangu heshima, kitu kidogo ashaambia mama yangu."

Karanja aliomba msamaha kwa jinsi alivyomkosea mpenzi huyo wake na kubainisha kuwa pia yeye aliwahi kumkosea vibaya.

"Naomba msamaha, sikufanya nikitaka. Pia wewe umenifanyia matendo.Mbona ulikuwa unapatia huyo mwanaume huyo simu anitusi? Nilikuwa nakupenda. Nilikuwa nafanya hayo juu ya mapenzi," Karanja alisema.

Moreen hata hivyo alimwambia, "Wewe move on na maisha yako" na kukata simu.

Karanja alikiri kwamba mpenziwe huyo amemtendea maovu mengi ingawa alikuwa anampenda kwa moyo wake wote.

Kuhusu kumripoti kwa polisi, alisema mwanadada huyo alikuwa ametoa vitu vyake kwa nyumba na kumsukuma kuchukua hatua hiyo.

"Nitamwambia what comes around goes around. Atakaa chini lakini ataona kuna mwenye alikuwa anafaa. Nilikuwa nakupenda lakini kilichofanyika ni sawa," Karanja alisema.

Gidi alishauri watu dhidi ya kuwapa moyo wote wasichana wa umri mdogo wa miaka 20-21.

Je, ushauri wako ni upi?