Patanisho: Mwanadada amwambia mama mkwe yeye si mfanyikazi baada ya kuagizwa awalishe ng'ombe

Momanyi alibainisha kuwa mke wake hakuwa anajiskia vizuri mnamo siku ambayo alikataa agizo la mama mkwe.

Muhtasari

•Momanyi alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka miwili baada ya kuzozana na mama mkwe alipomuagiza awapatie ng'ombe chakula na maji.

•Mary alipopigiwa simu alikataa katakata kuzungumza  na mumewe.

Image: RADIO JAMBO

Alhamisi asubuhi, jamaa aliyejitambulisha kama Ezra Momanyi ,28, kutoka Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Mary Mosoti ,23, ambaye alitoroka nyumbani baada ya kukosana na mama mkwe.

Momanyi alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka miwili baada ya kuzozana na mama mkwe alipomuagiza awapatie ng'ombe chakula na maji.

"Nilikuwa naamka naenda kazi. Nilikuwa naacha bibi nyumbani. Mama mkwe akamwambia apee ngombe maji na majani. Akamwambia mama mkwe yeye sio mfanyikazi. Kurudi kutoka kazini nikapata bibi ashatoka na watoto. Kumpigia simu hashiki, akishika anakata. Hadi wa leo sijaweza kumpata," Momanyi alisimulia.

Momanyi alibainisha kuwa mke wake hakuwa anajiskia vizuri mnamo siku ambayo alikataa agizo la mama mkwe.

"Mama nikimpigia simu anasema niambie bibi yangu hana shida na yeye arudi nyumbani. Hiyo siku ni kama alikuwa mgonjwa ndio maana alikataa," alisema.

Mary alipopigiwa simu alikataa katakata kuzungumza  na mumewe.

'Mimi sina la kumwambia!" Mary alisema na kukata simu mara moja.

Momanyi alisema, "Anakuwanga hivyo huwa anakata simu. Dawa ya kumpata nitafanya aje?Mama anaweza kumpigia. Nitamwambia ampigie."

Wakati alipopewa fursa ya kuzungumza na Mawr hewani, Momanyi alimwambia, "Mary mimi nakupenda naomba urudi tukae pamoja nyumbani tusaidiane vile tulikuwa tunasaidiana."

Je, una maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?