Patanisho: Jamaa amtumia mpango wa kando Sh 2000 baada ya kuiba Sh 4000 za mkewe

Hellen alifichua kwamba alitukanwa vibaya na mpango wa kando wa mumewe wakati alipompigia simu.

Muhtasari

•Chumo alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilivurugika baada ya mkewe kuchukua simu yake alipopigiwa na mpango wa kando.

•Hellen alifichua kwamba kabla ya tukio hilo alikuwa amepoteza shilingi elfu nne ila mumewe alidai hakuziona.

Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Mathew Chumo ,31, kutoka Uasin Gishu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Hellen Chepkirong ,29, ambaye alimuacha mwezi uliopita baada ya kugundua ana mpango wa kando.

Chumo alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilivurugika baada ya mkewe kuchukua simu yake alipopigiwa na mpango wa kando.

"Tulikosana na bibi wakati ambao alinifumania na mpango wa kando. Kuna mrembo nilikuwa naye akanipigia simu usiku nikiwa na mke wangu. Mke wangu alikashika simu akaongea na yeye mpaka wakafikia hatua ya kutusiana naye. Mke wangu alikasirika alafu kesho asubuhi akafunga virago akaenda," Mathew alisema.

Aliendelea, "Kuna kazi nilikuwa nafanya town ndipo tukakutana na huyo mrembo na akanipea number yake tukaanza kuongea. Unajua shetani huingia watu. Naomba unisaidie turudiane. Nimejaribu kumpigia lakini ameniweka blacklist. Nilijaribu kuongea na ndugu yake akaniambia wataongea. Huyo mrembo alikuwa anaitwa Mercy."

Hellen alipopigiwa simu alikiri kuumizwa sana moyoni na mzazi huyo mwenzake na akafunguka kuhusu alivyogundua ana mpango wa kando.

"Huyo alikuwa mume wangu. Sasa mtu akikusumbua, si inabidi uachane na yeye. Amenisumbua sana!! Mimi sikushika simu ya huyo mrembo, yeye mwenyewe alishika simu wakaongea. Baadaye nikamuuliza na nani akasema wanaongea na dada yake Mercy.

Wakati alipotoka nje, message ikawa imeingia kwa simu yake. Sijui ni shetani gani alinifanya nisome message, ilisema 'Beb ile pesa ulituma 2000 imeisha, unaweza nitumia ingine?" Hellen alisema.

Hellen alifichua kwamba kabla ya tukio hilo alikuwa amepoteza shilingi elfu nne ila mumewe alidai hakuziona.

"Nilikuwa nimepoteza shilingi elfu nne kwa nyumba nikamuuliza akasema hajui. Alituma 2000 akabaki na yake 2000. Nitaishi aje na mtu kwa nyumba nikificha pesa. Pesa yangu ulitumia mrembo. Nilipomuuliza alisema iko tu hivyo iko. Nilimwambia maisha tu itaendelea," alisema.

Aliongeza, "Baadaye nilitoa hiyo number ya huyo mrembo kwa simu yake.Nilipompigia huyo mrembo, si alinitusi. Watu si wako na matusi!! Ameninyanganya mzee, akakula pesa yangu na bado anitusi!! Hiyo kitu iliniuma sana. Huyo mrembo ata aliniambia yeye sio Mercy"

Chumo alikiri kwa mkewe kuwa na mpango wa kando na kuapa kuwa tayari ameachana naye na kufuta namba yake.

"Mimi nakupenda, wacha tusameheane. Nimekubali makosa yangu naomba unisamehe. Ukiona nimeenda Radio Jambo jua mambo yameumana,"  Chumo alimwambia mkewe.

Mercy alimwambia, "Sijaamini kama umebadilika. Wewe ni Mkristo na ukawa na mpango wa kando! Ungekuwa unanipenda hungekuwa na mpango wa kando. Atanipatia muda roho itulie. Hiyo kitu ni ngumu sana. Unipatie kama mwezi hivi. Kumsamehe nilikusamehe, nilikasirika ikaisha."

Chumo hata hivyo hakuridhika na muda wa mwezi mmoja ambao mkewe aliomba na hivyo akamuomba apunguze.

Ni sawa basi. Ajaribu basi, majukumu ya nyumba awajibike kama baba," Mercy alisema.

Hellen pia alisikika baada ya mumewe kumuita 'My dear', jina ambalo alikiri hajawahi kuitwa tena naye.

Chumo alimwambia, "My dear mi nakupenda. Kuja tuishi kama vile tulikuwa. Nakupenda kama njugu moto."

Hellen alisema, "Mi unajua nilikuheshimu kama mume wangu, nilikupenda lakini ulinikosea sana. Nilikusamehe kitambo. Nitarudi tu."

Je, una ushauri upi kwa wawili hao?