Patanisho: Jamaa ataka Gidi atangaze namba yake apate Mkamba mrembo baada ya kuhangaishwa na mpenziwe

"Nikipata mwanamke Mkamba ambaye ako na kazi, mwanamke mzuri na mrembo, itakuwa sawa," John alisema.

Muhtasari

•Doreen alidai  kwamba aligura mahusiano yake baada ya mpenziwe kufanya mimba yake itoke kisha akamfukuza.

•John alitoa ombi maalum kwa Gidi amsaidie kupata mwanadada wa matamanio yake na hata akatoa sifa anazotaka.

Image: RADIO JAMBO

Ijumaa asubuhi, mwanadada aliyejitambulisha kama Doreen Odhiambo mwenye umri wa miaka 20 alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake John Matagaro ,35, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Doreen alidai kwamba aligura mahusiano yao ya chini ya mwaka mmoja mwezi Agosti mwaka huu baada ya mpenziwe kufanya mimba yake itoke kisha akamfukuza. Alisema walikuwa katika mikakati ya kupata mtoto pamoja. 

"Tulikuwa tunaishi na yeye. Nampenda, sipendi kumshuku lakini yeye ananishuku sana. Anasema anashuku kuna wanaume. Nashindwa kumuelewa. Saa hii niko kwetu, nilitoka hivi majuzi. Aliniambia nitoke amemove on," Doreen alisema kabla ya simu yake kukatika.

Gidi alijaribu kumtafuta mwanadada huyo kwa simu mara kadhaa lakini kwa bahati mbaya hakuweza kupatikana tena.

Hata hivyo, mtangazaji huyo mahiri aliendelea kumtafuta Bw. John ili kusimulia hadithi yake.

"Niko na watoto hapa nyumbani. Saa hii, yeye ni kama bibi wa tatu. Nilimwambia wa kwanza alienda akaniachia watoto, wa pili alienda Saudia, yeye ni wa tatu. Hataki niongee na huyo wa Saudia. Aliharibu simu, nilienda nikachukua ya loan. Anataka aharibu simu ya wenyewe na sijalipa. Niliona kama hajakomaa. Siri ya nyumbani anaambia wanarika wake. Aliniambia anaenda kwao, hakuniambia," John alisimulia.

Aliendelea, "Huyo ambaye alienda Saudia ni bibi wa pili. Alinitumia 5,000 nikanunua simu. Jana ndio aliniambia nikae na bibi yangu. Bado nina imani kwamba akirudi Kenya atanirudia tena. Huwa tunaongea naye. Wakati alienda alitumia kitambulisho changu kama mke wangu. Wakati alienda tulikuwa pamoja, alikuwa anatuma pesa ikafika mahali akaacha. Doreen miaka yake ni kidogo, bado hajakomaa. Mimi niko 35 hivi. Nilimwambia akifikisha 26 ndiyo atakomaa akili. Kwa sasa wacha nipumzike kidogo bila mke  kwanza niangalie hii mambo ya dunia. Maisha imekuwa ngumu sana."

John aliendelea kufunguka kuhusu jinsi Doreen amemhangaisha katika mwaka mmoja ambao wamekuwa na mahusiano.

Kufuatia masaibu hayo, alitoa ombi maalum kwa Gidi amsaidie kupata mwanadada wa matamanio yake na hata akatoa sifa anazotaka.

"Sasa hivi mimi nikipata mwanamke Mkamba ambaye ako na kazi, mwanamke mzuri na  mrembo, itakuwa sawa. Hata unaweza kupatiana namba yangu hapo ama nitafute kwa Facebook," John alisema.

Gidi hata hivyo alimshauri atafute mwanamke ambaye anataka na aweze kutulia.

Huku patanisho ikienda kuisha, John alitoa ujumbe kwa Doreen, " Bado mimi nampenda lakini miaka yake ni mchanga. Wacha atafute rika yake wamuoe."

Je, una ushauri gani kwa wawili hao?