Patanisho: "Depression zitaniua!" Jamaa aliyemwambia mkewe anajuta kukutana naye amlilia arudi

"Nimesoma lesson kubwa ya maisha. Nimepitia mateso ya moyo. Nateseka sana, hata kukula na kunywa inakuwa ni shida!" alisema Benson.

Muhtasari

•Benson alisema mkewe aligura ndoa yao ya chini ya mwaka mmoja mapema mwezi huu kutokana na makosa yake ya awali.

•"Chenye naogopa sana ni kumpoteza. Hicho ni kitu naogopa zaidi. Hata kama nilikuwa na makosa kubwa aje anisamehe," Benson alisema.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Jamaa ambaye alijitambulisha kama Benson Muli ,27, kutoka Eldoret alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Mercy Mueni ,26, ambaye alikosana naye siku kadhaa zilizopita kufuatia mzozo wa kinyumbani.

Benson alisema mkewe aligura ndoa yao ya chini ya mwaka mmoja mapema mwezi huu kutokana na makosa yake ya awali.

"Ilikuwa makosa ya kitambo. Nilidhani imeisha. Tulizungumza na tukasameheana.Baadae nilienda kazini kurudi nikapata amechukua vitu akaenda. Kumpigia simu alianza kunikumbusha jinsi nilimtusi, nikampiga na nilkachapa mtoto. Tuliombana msamaha, akanisamehe," Benson alisimulia.

Aliongeza, "Kabla aende, kuna wakati nilimpigia simu usiku nikamwambia najuta sana kwa nini nilikutana na yeye. Wakati alipoenda alisema ameenda ndo niache kujuta. Ni hasira  ilifanya niseme hivyo. Nilidhani makosa yameisha. Nakubali niko na makosa mengi. Nimejaribu kumuongelesha mara anasema atatafuta muda akuje tuongee, mara anasema nimpatie miezi miwili, mara anasema nioe mke mwingine.

"Huwa nampigia simu hadi usiku, siku ingine alisema nampigia simu usiku nikimuonyesha ni kama ako na wanaume wengine. Wazazi wake wananijua. Nilijaribu kutuma wazazi kwao lakini kitu ikatokea kwao," alisema.

Bi Mercy Mueni alipigiwa simu ila punde baada ya kuskia anataka kupatanishwa akakata mara moja.

Benson alisema, "Chenye naogopa sana ni kumpoteza. Hicho ni kitu naogopa zaidi. Hata kama nilikuwa na makosa kubwa aje anisamehe."

Alimwambia mkewe, "Mueni mahali uko naomba tu, najua nilikukosea makosa mengi lakini nakuomba sana uweze kunisamehe. Nakuahidi 100% nitabailikia. Nimesoma lesson kubwa ya maisha. Nimepitia mateso ya moyo. Nateseka sana, hata kukula na kunywa inakuwa ni shida!"

Je, ushauri wako ni upi?