• Salome alipopigiwa simu, mamake ndiye alishika simu na akasema kwamba mwanawe yuko mbali kidogo na yeye ndiye alikuwa na simu yake akiwa katika sehemu za Nyang’or.
Katika Patanisho ya kwanza ya mwaka 2024 kwenye stesheni ya Radio Jambo, mzee mwenye umri wa miaka 64 kwa jina James Yego kutoka Njoro Nakuru alitoa ombi kwa Gidi na Ghost kumpatanisha na mkewe Salome Yego mwenye umri wa miaka 54.
Bwana Yego alisema kwamba wameishi na mkewe kwa ndoa kwa miaka 37 lakini alitoka nyumbani takribani miezi miwili kwenda kwao nyumbani sehemu za Kisumu na tangu hapo hajawahi rudi.
“Dabake aliaga akaenda matanga akamaliza miezi 2 na akarudi tena kidogo akaenda tena makumbusho na hajarudi sijui shida ni gani, niko na watoto na yeye ndiye mlezi…” Mzee Yego alisema.
Hata hivyo alisema kwamba katika kipindi cha miaka 37, hii ni mara ya pili anamfanyia hivyo na sasa ameshindwa kwa nini amekaa mbali hivyo hali ya kuwa anajua nyumbani kuna watoto wanafaa kupangwa kuenda shule na mzee apate nafasi ya kutafuta riziki.
“Nimeongea na yeye jana asubuhu ananiambia atakuja na hakuji… imekuwa siku nyingi akisema hivyo na hakuji….miaka yote 37 tumeishi na yeye, hii ni mara ya pili… mara ya kwanza alienda kidogo baada ya kukosana nikafuatilia nikamrusdisha… sasa amekaa miezi miwili,” alisema mzee.
Salome alipopigiwa simu, mamake ndiye alishika simu na akasema kwamba mwanawe yuko mbali kidogo na yeye ndiye alikuwa na simu yake akiwa katika sehemu za Nyang’or.
Mamake Salome alimtetea bintiye kukaa nyumbani kwa muda mrefu bila kurudi kwa mume wake na watoto akisema kwamba ni lazima asalimie na hata hakuna haja ya kuharakisha kurudi nyumbani kwani hakuacha watoto wadogo bali ni watu wazima.