Patanisho: Jamaa ajipa matumaini baada ya mpenzi aliyemuacha 2022 kumtafuta awanunulie chips

Jackson alisema uhusiano wao ulisambaratika Februari 2022 baada ya simu yake kuharabika na kupelekea matatizo ya mawasiliano.

Muhtasari

•Jackson alifichua kuwa hivi majuzi Bi Brenda alimtafuta kupitia kwa rafiki yake na kumpa matumaini, lakini akaja kugundua kuwa walikuwa wanataka chips tu.

•"Kuna rafiki yake alinipigia akaniambia ati Brenda alikuwa anataka kuongea na mimi. Baadaye nikampigia akaniambia ati huyo msichana alikuwa anataka niwanunulie chipo," alisema.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Bw Jackson Luya ,27, kutoka Donholm alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Brenda Achieng ,25, ambaye alikosana naye takriban miaka miwili iliyopita.

Jackson alisema uhusiano wao wa miaka mitatu ulisambaratika Februari 2022 baada ya simu yake kuharabika na kupelekea matatizo ya mawasiliano.

"Mwaka wa 2022, tulikosa mambo ya mawasiliano. Nilikuwa shule Eldoret na yeye alikuwa shule meru. Simu yangu ilikanyangwa na gari mawasiliano yakakatika. Baadaye nilifanikiwa kupata katululu.Nilijaribu kumweleza simu ilivunjika lakini alikuwa ananishuku kila wakati. Nilimwambia siwezi kumfanyia vibaya," Jackson alisimulia.

Aliongeza, "Mwezi wa nane ndio nilipata simu. Akwa ananishuku niko na mtu. Baadaye Novemba akaanza kununa. Nikimpigia simu akawa yuko moodless. Mara anasema yuko busy. Tukawa tunaulizana kama mtu amemove on lakini hatuelewani." 

Jackson alifichua kuwa hivi majuzi Bi Brenda alimtafuta kupitia kwa rafiki yake na kumpa matumaini, lakini akaja kugundua kuwa walikuwa wanataka chips tu.

"Kuna rafiki yake alinipigia akaniambia ati Brenda alikuwa anataka kuongea na mimi. Baadaye nikampigia akaniambia ati huyo msichana alikuwa anataka niwanunulie chipo," alisema.

Aliongeza, "Huwa naskia mtoto akilia, ananiambia ni wa dada yake. Nashuku ni wake lakini ata kama ana mtotot mimi sina shida. Niko tayari kukaa naye hivyo.Tulikuwa tumeweka ahadi na yeye tutalindana. Hadi nilimleta kwetu.Novemba nilimtumia fare akakataa kuja."

Brenda alipopigiwa simu alisikika akisita kuongea na Jackson hewani. Alidai kwamba tayari walikuwa wamezungumza na kuelewana.

Jackson hata hivyo alisema, "Jana alinipia simu akiniuliza kama nimepoteza matumaini. Nikamwambia mimi sina shida.Nikamwambia niko sawa lakini ningependa kujua msimamo wake. Alisema nijifanye tu lakini kuna siku nitamhitaji."

Brenda alisema, "Kwani alitaka tuelewane aje. Yeye ndiye anafaa kuja na msimamo wake."

Jackson alisema, "Nataka kujua msimamo wake kwa sababu nakupenda.Nakupenda na nataka uwe mke wangu. Ningependa tuwe pamoja mpaka siku ya kutoka duniani."

Patanisho hiyo hata hivyo iligonga mwamba kwani simu ya Brenda ilikatika kwa mara ya tatu.

Je, maoni ama ushauri wako ni gani?