Patanisho: "Alisema akikufa nisiende kumzika" Mke amfokea mumewe baada ya ndoa ya miaka 25 kusambaratika

Bi Mwende alikiri kuumizwa na tabia ya mumewe kumsema vibaya kwa marafiki na jamaa zake.

Muhtasari

•Bw Nguki ambaye ni dereva wa trela alisema mkewe kwa njia tatanishi miezi michache baada ya mama yake kuaga na kuzikwa.

•"Hakuna mtu utaleta huko, huko ni kwangu. Nitarudi nikitaka. Apunguze ujinga na aheshimu baba yangu," Bi Mwende alimwambia mumewe.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Mwanaume aliyejitambulisha kama Ken Nguki (49)  kutoka kaunti ya Makueni alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Josephine Mwende (44) ambaye aligura mwaka wa 2022 baada ya miaka 25 kwenye ndoa.

Bw Nguki ambaye ni dereva wa trela alisema mkewe kwa njia tatanishi miezi michache baada ya mama yake kuaga na kuzikwa.

"Bibi aliondoka kwa njia tatanishi baada ya kuzika mamake. Alienda kutafuta kazi bila kunijulisha. Babake alikatiza hiyo kazi nilipomwambia. Baadaye wakati wa uchaguzi aliingia kwenye kampeni akaanza kutembea na watu wa siasa," Bw Nguki alisimulia.

Aliongeza, "Baadaye alikuwa anakuja nikiwa kazini anachukua kila kitu anataka. Alibeba kila kitu yake akaenda. Siku hizi akitoka mahali anafanya kazi huwa anaenda kwao. Huwa anaongea na watoto tu kwa simu. Alitoka kimya kimya."

Nguki alisema kwamba baada ya kufuatilia aligundua kuwa baba mkwewe ndiye aliyemshauri bintiye aondoke kwa madai kuwa hakuwa akimshughulikia.

"Baba mkwe aliniambia baadaye kuwa yeye ndiye alimtoa. Alisema ati bibi yangu alimwambia huwa simsaidii ati huwa nasaidia watoto tu. Hapo wali nilikuwa nimempatia ATM yangu na hata pin. Babake aliniambia yeye ndiye alimtoia na yeye ndiye atamrudisha. Niligundua kumbe hii ndoa ilikuwa imeshikiliwa na mama mkwe. Nataka anipee way foward, nitafute bibi ama aseme kilichomtoa kwangu," alisema.

Bi Mwende alipopigiwa simu alilalamika vikali kuhusu baba huyo wa watoto wake watano akidai kwamba amekuwa akimtusi  na kumsema vibaya kwa watu wake wa karibu.

"Mtu anakwandikia meseji anakuita malaya, anasema nisiwahi kanyanga kwake atazikwa na watoto, huyo ni mume kweli? Akiwa na shida anataka nimsaidie. Wakati mwingine anapigia dada zangu anawaambia nalala na watu wa malori. Aliita dadangu mdogo wakashiriki kikao ambapo alimwambia mambo mabaya kunihusu Kuna siku alichukua simu ya mwanamke akaniandikia meseji," BI Mwende alifunguka.

Kwa hasira nyingi aliendelea, "Aachane na mimi, alisema akikufa nisiende kumzika. Kila mtu ashughulike na maisha yake. Kabla nitoke kwake, nilikuwa mgonjwa miezi sita, hakuwa ananishughulikia. Hilo lilimkasirisha sana baba yangu."

Aidha, Bi Mwende alimuonya mzazi huyo mwenzake dhidi ya kuoa mwanamke mwingine akimbainishia kuwa bado ni kwake

"Hakuna mtu utaleta huko, huko ni kwangu. Nitarudi nikitaka. Apunguze ujinga na aheshimu baba yangu," alisema.

Wawili hao hata hivyo hawakuweza kupatana na illishia kwa Bi Mwende kumwagiza mume huyo wake amfuate kwao ili kusuluhisha mzozo wao.

Je, ushauri wako ni upi?