Patanisho: Mke auza kondoo kwa bei ya kutupa baada ya kufukuzwa kwa kuzozana na wakwe zake

Alidai kuwa ndugu za mumewe walimfanyia madharau sana na kusababisha yeye kufukuzwa nyumbani.

Muhtasari

•Francisca alisema ndoa yake ya miaka 4 ilivunjika Agosti mwaka janaa baada ya mvuragono kutokea kati yake na wakwe zake.

"Aliniambia niende kwetu. Nilikuwa na mbuzi, akasema niuze niende nyumbani. Ilikuwa kondoo 7, nikauza 23,000 nikaenda nyumbani," Francisca alisema.

Image: RADIO JAMBO

Mwanadada ambaye alijitambulisha kama Francisca Chepchumba ,22, kutoka kaunti ya Elgeyo Marakwet alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake James Njoroge ,33, ambaye alikosana naye mwaka jana.

Francisca alisema ndoa yake ya miaka 4 ilivunjika Agosti mwaka janaa baada ya mvuragono kutokea kati yake na wakwe zake.

Alidai kuwa ndugu za mumewe walimfanyia madharau sana na kusababisha yeye kufukuzwa nyumbani.

"Saa hii niko kwao Nakuru lakini amekataa kurudi nyumbani.Nilikaa nyumbani kwetu miezi sita. Nikatafuta nauli nikarudi mwenyewe. Hata hivyo, alisema hanitaki na watoto wanguakasema hatarudi. Alisema atanitumia kila kitu lakini hatarudi nyumbani," Francisca alisimulia.

Aliongeza, "Kwa sasa ako pande za Marigat. Tayari ameniambia nitafute mtu mwingine. Huwa anatuma pesa ya mahitaji. Nikimwambia sina kitu anatuma lakini hatuongei. Hatuna amani nyumbani. Bado roho yangu inamhitaji."

Kuhusu mzozo ambao ulisababisha yeye kufukuzwa na mumewe, mwanadada huyo alisimulia, "Dadake na ndugu yake kuna mambo ilikuwa inatokea tunagombana. Tulikuwa tunaishi karibu tu nao, sio mbali. Nilikuwa nimeacha mtoto na dada yake nikaenda mahali, niliporudi nikapata mtoto amelia sana. Nikamuuliza mbona mtoto analia akiwa, nillimtusi nikamwambia ata yeye atakuwa na mtoto wake na atakuwa na mjukuu. Mzazi alipigia mzee akamwambia nimetusi dada yake. Akanipigia akaniuliza mbona nimeenda nyumbani kutusiana. Akaniambia niende kwetu. Nilikuwa na mbuzi, akasema niuze niende nyumbani. Ilikuwa kondoo saba, nikauza nikaenda nyumbani."

Aliongeza, "Niliaenda nyumbani hatukuongea miezi tatu. Hakuwa anashughulikia watoto wakati huo. Haikuwa rahisi kukaa nyumbani na wazazi, alikuwa amenitoa shule, kidato cha nne wakati wa Corona. Akakataa nirudi shule akasema kama nataka kurudi hatanioa. Hatuelewani vile niliuza hao mbuzi wake. Siku moja alinipigia kama nilibakisha pesa ya hao mbuzi niliuza. Wote niliuza 23,000."

Bw James alipopigiwa simu, alionyesha wazi kwamba hataki kuzungumza na mkewe kwani alikata simu na kuizima.

Simu ya Francisca pia ilizimika na hakupatikana tena. Kufuatia hayo, wawili hao hawakuweza kupatana.

Je, ushauri wako kwa mwanadada huyo ni upi?