Patanisho: Mwanadada aomba radhi baada ya mumewe, ex wake kuzozania nani ni baba wa mtoto wake

Clare alikiri kwamba aliwahi kumwambia mzazi huyo mwenzake kuwa mtoto sio wake kutokana na hasira.

Muhtasari

•Clare alisema ndoa yake ilivurugika baada ya familia yake kuingilia na kumtaka atengane na baba huyo wa mtoto wake.

•Cyrus alilalamika kuhusu suala la Clare kumwambia mtoto sio wake, jambo ambalo alikiri lilimuathiri.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Clare Awour ,23,  kutoka  Eldoret alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mzazi mwenzake Silas Mwanda ,28 ambaye alikosana naye baada ya ndoa ya mwaka mmoja.

Clare alisema ndoa yake ilivurugika baada ya familia yake kuingilia na kumtaka atengane na baba huyo wa mtoto wake. 

Alikiri kwamba alimuongelesha vibaya mpenziwe baada ya kutengana na akabainishwa kwamba kila mtu ame'move on.

"Niliishi na Cyrus mwaka moja. Akawa anazungumza na msichana mwingine, walikuwa wakiongea kuhusu jinsi huwa wanapatana kwa lodging. Nikaambia familia yangu alafu familia yangu, hasa mamangu akaniambia nitoke," Clare alisimulia.

Aliendelea, "Wakati huo nilikuwa nimejifungua. Labda ndio maana alikuwa anatafuta msichana mwingine.  Familia yangu tayari ilikuwa imemchukia. Familia yake wanajua tuko pamoja. Lakini nikirudi huko familia yangu wananiambia nisiwahi rudi nyumbani kama nimeamua kurudi kwake."

Clare zaidi alikiri kwamba aliwahi kumwambia mzazi huyo mwenzake kuwa mtoto sio wake kutokana na hasira.

"Kuna wakati alikuwa ananitext, hizo jumbe zilikuwa zinaniuma. Nilimtusi na nikamtumia jumbe mbaya. Sasa ameniblock hadi kwa Facebook.

Hadi nilimwambia mtoto si wake na ni wake. Tangu mtoto azaliwe hajawahi kumshughulikia. Aliniambia atakuja kuiba mtoto," alisema.

Aliendelea, "Nataka tu nimuombe msamaha niitoe kwa roho yangu, sitaki turudiane. Nataka anisamehe kwa sababu barabara huwa napita nikienda kanisa tunakutana. Na hatuongei."

Cyrus alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba hana shida na mzazi huyo mwenzake.

Hata hivyo, alilalamika kuhusu suala la Clare kumwambia mtoto sio wake, jambo ambalo alikiri lilimuathiri.

"Pia mimi imekuwa ikinisumbua. Ilifika mahali mimi nikashindwa kabisa... Mimi sina shida na wewe kabisa kabisa. Nimebaki kukubali vile uliamua. Mimi naendelea na maisha yangu tu," Cyrus alisema.

"Ilifika wakati hadi anapea jamaa mwingine aniambiie mtoto sio wangu. Ilifika mahali hadi mimi nikaanza kushuku sio wangu. Wakati Clare alipata mtoto, kuna jamaa alianza kudai mtoto ni wake. Mimi nikijaribu kufuatilia ni nani ikawa shida. Niling'ang'ana  kumfuatilia hadi nikashindwa."

Nilikuwa nampenda. Mimi sijawahi kuamua chochote kile. Ni maneno ya watu tu. Mimi sina shida na huyo msichana," aliongeza.

Clare alisema, "Mtoto ni wa Cyrus. Ni ugomvi tu ulifanya nimwambie hivyo. Jamaa ambaye alizungumza naye ni ex-boyfriend lakini mtoto sio wake. Alikuwa ananitext tu lakini hatukuwa tunakutana. Niko sure mtoto ni wake. Niko tayari kwa DNA kama anataka. Lakini mtoto ni wake."

"Asante kwa kunisamehe. Nilikuwa nataka tu hiyo chuki initoke," alimwambia Cyrus.

Cyrus kwa upande wake alimwambia, "Pia mimi sina chuki na wewe. Ata watu wa kwenu nilikuwa nawapenda. Lakini yaliyotokea nakubali. Kama mtoto ni wangu basi nitamsaidia."

Cyrus alidokeza kwamba yuko huru kurudiana na mzazi huyo mwenzake. Clare kwa upande wake alimsihi ashughulikie mtoto.

Je, una maoni yepi kuhusu Patanisho ya leo?