Patanisho: Jamaa atoboa ukuta ili kuchungulia kakake na mkewe wakishiriki mapenzi

Evans alikiri kwamba alimchungulia nduguye na mke wake, ila akadai kwamba sio yeye alitoboa shimo.

Muhtasari

•Evans alisema uhusiano wake na Chris uliharibika Februari mwaka huu wakati ndugu huyo wake alipomsingizia alichochea mke wake kuondoka.

•Chris aliweka wazi kwamba hataki uhusiano wowote na mdogo huyo wake kutokana na mambo ambayo amefanya.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Evans Juma ,24, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na ndugu yaje Chris Juma ,28, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Evans alisema uhusiano wake na Chris uliharibika Februari mwaka huu wakati ndugu huyo wake alipomsingizia alichochea mke wake kuondoka.

"`Ndugu yangu alisema nilimchochea na mkewe. Alileta vurugu akata tupigane lakini nikatoroka. Yeye ndiye aliyenileta Nairobi. Mke wake alikuwa mtu social sana. Tulikuwa tunaongea tu stori za kawaida. Ndugu yangu akasema nilichochea yeye kuachana na mkewe," Evans alisema.

Jamaa huyo alisema nduguye pia alimshtumu kwa kumchungulia yeye na mkewe wakiwa katika nyakati za kimapenzi.

Alikiri kwamba alimchungulia mke wa nduguye, ila akadai kwamba sio yeye alitoboa shimo.

"Baadaye alikuja kusema nilitoboa shimo kwa nyumba ya mabati nilikuwa nachungulia akiwa na mkewe. Sikutoboa shimo lolote kwa mabati. Nilipata nyumba ikiwa hivyo. Shimo ilikuwa lakini sio mimi nilitoboa. Kweli nilichungulia kidogo," alisema.

Aliongeza, "Hatuongei na ndugu muda mrefu. Alitaka tupigane lakini nikatoroka nikaenda kwa rafiki yangu. Sijui kama mke wake amerudi."

Chris alipopigiwa simu alisisitiza kwamba nduguye alitoboa ukuta wa nyumba na kumchungulia yeye na mkewe.

Aliweka wazi kwamba hataki uhusiano wowote na mdogo huyo wake kutokana na mambo ambayo amefanya.

"Huyo kijana mambo yake sitaki kusikia. Kwa heshima ya Patanisho, sitaki kuongea na yeye," Chris alisema.

Aliongeza, "Amekuwa kizungumkuti kwangu binafsi na kwa familia, hata kwa kijiji kizima. Baada ya wazazi wake kufariki nilimchukua nikamleta mjini, ila akawa kikwazo.Nilikuwa naishi kwa chumba kimoja, tukahamia katika chumba cha vyumba viwili,alienda katika kile chumba akabomoa bati."

Chris pia alimshtumu nduguye kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe huku akidai aliwahi kuwafumania.

"Nilimkuta na mke wangu. Mke wangu alikuwa anaoga kwa nyumba, akawa anamchungulia. Wakati mmoja nilimfumania mke wangu akiwa tupu, na jamaa pia alikuwa tupu," alisema.

"Nilimtoa nyumbani kama anaiba, Sasa hivi nishamchoka. Kuku wa jirani akipotea, manyoya yanapatikana nyumbani kwetu," alisema.

Evans alisema, "Kuchungulia nilichungulia kidogo, lakini kunipata na mkewe hakuna kitu tulikuwa tunafanya.. Naomba unisamehe, nilikosa. Nanyenyekea mbele ya Wakenya. Rudisha roho yako chini unisamhe. Niunblock tuwe tunaongea."

Chris alimwambia, "Muombe Mwenyezi Mungu msamaha sio mimi.  Kwa sababu ya Gidi na Ghost mimi nimeamua kukusamehe. Badilika nakuomba."

Je, ushauri na maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?