Patanisho: Jamaa ajuta kumtukana mama mkwe baada ya kukosana na mkewe

“Nilikuwa nataka tu kumuomba msamaha mama mkwe, msichana wake tuliachana. Sitaki kurudiana na msichana wake, nataka tu msamaha kwa mama mkwe juu nilimtusi kutokana na hasira. Ni vile alikuwa anaingilia ndoa yangu na bintiye,”

Muhtasari

• Hata hivyo, Eric alisema lengo lake ni kumuomba tu msamaha mama mkwe wala hana nia ya kurudiana na binti yake.

• “Mwambie akuje nyumbani, lakini alinitusi vibaya sana. Mimi sina shida na yeye, aje nyumbani ndio aombe msamaha vizuri,” Nduku alisema.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho kwenye Gidi na Ghost Asubuhi ndani ya Radio Jambo, kijana kwa jina Eric Mutua mwenye umri wa miaka 26 kutoka Kitui aliomba kupatanishwa na aliyekuwa mama mkwe wake, Nduku mwenye umri wa miaka 50.

Eric alieleza kwamba alikuwa anaishi na mkewe na baada ya kupata mtoto, akaamua kuenda kwao badala ya kwenda kwa kina Eric.

Baada ya kumuuliza mama mkwe Nduku, walijibizana na kutokana na hasira, Eric akajipata amemtamkia mama mkwe matusi, jambo ambalo limekuwa likimsuta nafsi yake na kutaka kumuomba msamaha.

“Nilikuwa naishi vizuri na mtoto wake tukazaa mtoto. Akaenda kwao badala aende kwetu, sasa kuuliza mama yake akaniambia eti mtoto alisema anataka kuenda huko juu ako na mtoto mdogo, sasa shida ikaanzia hapo, mama mkwe akaanza kuniambia mtoto ni wake,” Eric alisema.

Hata hivyo, Eric alisema lengo lake ni kumuomba tu msamaha mama mkwe wala hana nia ya kurudiana na binti yake.

“Nilikuwa nataka tu kumuomba msamaha mama mkwe, msichana wake tuliachana. Sitaki kurudiana na msichana wake, nataka tu msamaha kwa mama mkwe juu nilimtusi kutokana na hasira. Ni vile alikuwa anaingilia ndoa yangu na bintiye,” Eric alifafanua.

Kwa upande wake, mama mkwe alipopigiwa simu, alimtaka Eric kuzungumza Kikamba ili waelewano, akisema kuwa Kiswahili hawangeelewana vizuri, jambo ambalo Gidi na Ghost walikataa wakisema walikuwa kwenye redio.

“Mwambie akuje nyumbani, lakini alinitusi vibaya sana. Mimi sina shida na yeye, aje nyumbani ndio aombe msamaha vizuri,” Nduku alisema.