Patanisho: Jamaa agadhabika baada ya kugundua mke aliyeoa miaka 10 anapanga kuoelewa na mwingine

"Nilikuwa nimeoa Phanice. Tumeishi zaidi ya miaka 10. Tumepata watoto 3. Wakati moja nilitoka kazini nikapata anataka kuoelewa," Joel alisimulia.

Muhtasari

•Joel alisema ndoa yake ya miaka kumi ilisambaratika wakati alipomfukuza baada ya kupata anapanga kuolewa kwingine.

•Vanice alikubali kurudi kwa ndoa yake ila akatupilia mbali madai ya mumewe kwamba alikuwa na mpango wa kuolewa na mwingine.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Joel Wamukota alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Vanice ambaye alikosana naye takriban mwaka mmoja uliopita.

Joel alisema ndoa yake ya miaka kumi ilisambaratika wakati alipomfukuza baada ya kupata anapanga kuolewa kwingine.

"Nilikuwa nimeoa Phanice. Tumeishi zaidi ya miaka 10. Tumepata watoto watatu. Wakati moja nilitoka shule mahali nafanya kazi nikapata anataka kuoelewa," Joel alisimulia.

Aliendelea, "Nilikuwa nimemuoa rasmi. Ata nilipata barua nikatoa ng'ombe 4. Nilipata anapanga kuolewa. Niliona anaombwa direction ya kwao, nikamfukuza.  Nilikuwa na hasira, ningempiga ningemuumiza. Ako kwao lakini siongei na yeye, huwa naongea na mama namtumia pesa asaidie watoto.  Yeye huwa na matumaini ya kuja lakini nataka aape mbele ya Wakenya eti hatarudia. Kama hawezi kubadilika asirudi."

Vanice alipopigiwa simu, Joel alitumia fursa hiyo kumuomb a arudi, ila kwa masharti kwamba lazima abadilike.

"Nimekupatia ziaid ya mwaka moja. Kama umebadilika, urudi. Kama hujabilika, ukae kwenu. Nataka uape mbele ya watu milioni kwamba umebadilika," Joel alimwambia mkewe.

Vanice alikubali kurudi kwa ndoa yake ila akatupilia mbali madai ya mumewe kwamba alikuwa na mpango wa kuolewa na mwingine.

"Sikuwa napanga kuoa. Ni yeye mwenyewe tu ndiye aliniacha nikiwa mgonjwa. Alikuwa anarudi nyumbani saa tisa alfajiri na huwezi kumuuliza. Ukimuuliza anakuwa tu mkali," Vanice alisema.

Joel hata hivyo alisisitiza kwamba mkewe alikuwa na mpango wa kuolewa na akamshtumu kwa kumpigia kelele nyumbani na kumkosea heshima.

"Badilisha tabia yako, ujue mimi ni bwana yako nilitoa ng'ombe. Ukirudi kwako ujue sitaki kuishi chini ya mwanamke. Lazima uishi kwa maagizo ya mwanaume," Joel alimwambia mkewe.

Vanice alisema, "Kitu ilikuwa ya kitambo imeisha. Mimi nimekuwa mwaminifu na baada ya kutoka huko nilirudi kwa wazazi wangu."

Je, ungekuwa Vanice ungekubali kurudi kwa ndoa hiyo?