Patanisho: Kijana aliyempachika mimba msichana wa shule adai "shetani aliniingia"

“Sio eti nilitaka kupata mtoto. Ni shetani tu, sijui ni aje. Yeye anasisitiza anataka kutoa," Eric alisema.

Muhtasari

•Eric alisema mahusiano yake ya miaka miwili yalisambaratika hivi majuzi baada ya mkewe kudai kutia ujauzito wa miezi mitatu ambao anabeba.

•Kijana huyo aliendelea kudai kwamba hakuna jambo mbaya alilomfanyia mpenziwe ila kumshauri asitoe mimba.

The young man claimed that one can die at a young age and 

Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Eric Boiyo ,22, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Lizzy Chemutai ,19 ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Eric alisema mahusiano yake ya miaka miwili yalisambaratika hivi majuzi baada ya mkewe kudai kutia ujauzito wa miezi mitatu ambao anabeba.

Alisema mpenziwe alilalamika kuhusu kuwa mwanafunzi na kutokuwa tayari kuwa mzazi.

Alisema eti yeye ni mwanafunzi hako tayari,” Eric alisema.

Kuhusu sababu ya kumpachika ujauzito mpenziwe ilhali angali shuleni, kijana huyo alisema, “Si kupenda kwangu. Shetani tu aliniingia. Wakati wa tendo kuna vile unaweza kuhisi vizuri mpaka unasahau. Naomba mnisaidie asije akatoa.”

Eric alidai kwamba ana uwezo wa kushughulikia mtoto na kufichua kwamba anafanya kazi ambayo inampa shilingi elfu sita kila siku.

Alisema huenda mpenziwe tayari amem’block kwani hajaweza kuwasiliana naye siku kadhaa zilizopita. Alisema alijaribu kumshawishi mpenziwe asitoe mimba ila wakakosa kuelewana.

“Unajua huwezi ukajua kitakachotokea, anaweza akaenda kutoa mimba, labda akufe nipoteze watu wawili. Nitaenda kwao hivi karibuni,” alisema.

Kijana huyo aliendelea kudai kwamba hakuna jambo mbaya alilomfanyia mpenziwe ila kumshauri asitoe mimba.

“Hakuna kibaya nilimfanyia. Alikuwa ananiambia tuende hospitali akatoe mimba nikamzungusha. Hapo ndo ni kama alinikasirikia,” alisema.

Alidai kwamba mpenziwe bado atapata nafasi ya kuendelea na masomo hata baada ya kujifungua.

Aidha, alisema ingawa hakutaka kumpachika mimba mpenzi wake, anafurahi kupata mtoto ili awe na zao.

“Sio eti nilitaka kupata mtoto. Ni shetani tu, sijui ni aje.. Yeye anasisitiza anataka kutoa. Unajua maisha ya saa hii huwezi ukajua kesho. Unaweza ukafa mapema. Ni vizuri angalau uone umeachia mzazi wako mjukuu,” alisema.

Je, una maoni yepi kuhusu patanisho ya leo?