Patanisho: Jamaa amfumania mkewe na mwanaume nyumbani kwake, ataka arudi juu alikula mali yake

"Niliwapata live live kwa macho. Jamaa huyo ata aliniambia bibi yangu hanipendi na walikuwa naye hapo, na ni nyumba yangu," Richard alilalamika.

Muhtasari

•Richard alisema ndoa yake ya miaka sita ilivurugika baada ya kugundua mkewe ana mahusiano na  mwanaume mwingine.

•Richard alifichua kwamba baada ya Bi Esther kudai angependa kurudi, alimtumia nauli mara moja ila akakosa kuenda.

Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Richard Ondieki ,25, kutoka Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Esther Njoki mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikosana naye mwezi uliopita.

Richard alisema ndoa yake ya miaka sita ilivurugika baada ya kugundua mkewe ana mahusiano na  mwanaume mwingine.

Licha ya hayo, alisema angependa kurudiana na mzazi mwenzake kwani anahofia huenda watoto wao wakateseka.

"Bibi yangu tumeishi naye vizuri. Huwa nafanya kazi mchana lakini anashinda kwa nyumba.Kuna jirani ambaye alimtafutia kazi, sikujua kumbe alikuwa anamkatia. Niliwapata live live kwa macho. Kitu umeona sio kama ya kuambiwa," Richard alisimulia.

Aliendelea,"Jamaa huyo ata aliniambia kwamba bibi yangu hanipendi na walikuwa naye hapo, na ni nyumba yangu, mimi ndio nalipa kodi. Huyo jamaa aliendelea kuniambia maneno mabaya yenye siwezi kusema hewani. Mwanamke pia akasema amechoka anataka kuenda. Nikaona hakuna kitu nikafanya. Bibi alitoka, mimi nilihama nikawaachia nyumba. Walichukuana na jamaa wakahamia kwingine. Wakaachana mwanamke akarudi kwao. Baadaye huwa ananipigia simu akisema anataka kurudi. Lakini mtu hufikiria kwanza kabla achukue hatua. Nilitaka tu aniambie ukweli ako wapi. Nilitaka nimuombe msamaha kwa sababu ako na watoto wangu. Huyo mwanadada alikula mali yangu akaenda, naona tu arudi." 

Richard alifichua kwamba baada ya Bi Esther kudai angependa kurudi, alimtumia nauli mara moja ila akakosa kuenda.

Kwa bahati mbaya, Richard hakuweza kupatanishwa na mkewe kwani simu ya Esther haikuingia wakati Gidi alipompigia.

Richard alipopewa fursa ya kunena naye hewani, alisema, "Mama Wacera mimi sina ubaya na wewe. Mimi nakungojea niko tu sijaoa mwingine. Kama una hakika unataka kurudi, tafadhali nipigie simu tuelewane."