Patanisho: Mwanadada afungiwa nyumba baada ya 'kumfukuza' mumewe akidai anajiweza

Grace alikiri kwamba alishindwa kulipa kodi baada ya mumewe kuondoka, jambo lililofanya nyumba kufungwa.

Muhtasari

•Grace alidai ndoa yake ya miaka minne ilisambaratika mwaka jana baada ya nyumba yao kufungwa na mwenye nyumba.

•Kevin alifichua kwamba mkewe ndiye aliyemfanya aondoke nyumbani baada ya kudai kwamba angeweza kukaa pekee yake.

Image: RADIO JAMBO

Mwanadada ambaye aljitambulisha kama Grace Gacheri ,23, kutoka Mwihoko alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Kevin Chege ,26, ambaye alikosana naye mwaka uliopita.

Grace alidai ndoa yake ya miaka minne ilisambaratika mwaka jana baada ya nyumba yao kufungwa na mwenye nyumba.

"Tulikuwa tunakaa na yeye. Vile nyumba ilifungwa yeye alirudi nyumbani na mimi nikarudi kwetu. Huwa nashinda nikimuuliza anasema nimpatie muda. Lakini anasaidia mtoto. Wakati mwingine tunaelewana, wakati mwingine tunakorofishana," Grace alisimulia.

Aliendelea, "Nyumba ilifungwa mwaka jana na vitu zikafungiwa huko. Shida yake ni kulewa sana. Yeye ni mama boy. Anapenda kusikia mama sana. Ndio maana ako huko. Hataki kutoka. Mi nimechoka nataka kurudi kwangu."

Kevin alipopigiwa simu alibainisha kwamba angali anatafuta pesa za kujipanga kabla ya kumrejesha mkewe.

Aidha, alifichua kwamba mkewe ndiye aliyemfanya aondoke nyumbani baada ya kudai kwamba angeweza kukaa pekee yake.

"Nilimwambia angojee nipate pesa. Yeye ndo alifanya vitu zikapotea. Alikuwa anasema anataka kujikalisha nikamuachia vitu zote. Alikuwa amesema anajiweza nikamuachia. Baadaye nyumba ikafungwa," Kevin alisema.

Grace alimwambia, "Masiku bado zinasonga na nilitaka kujua msimamo wako juu huwa tunakosana kila wakati. Kama huko patient, unataka nifanye aje?"

Kevin alimjibu,"Siwezi kurudi hivyo wakati najaribu kununua vitu zingine."

Kuhusu sababu ya yeye kutaka kukaa pekee yake, Grace alisema, "Ilifika mahali yeye alikuwa anakuja wakiwa na marafiki wake wakiwa walevi kisha wanaanza vituko. Nilimwambia mimi nitajikalisha... Mi nataka kurudi nyumbani ndio niendelee na kazi zangu."

Je, ushauri wako kuhusu Patanisho ya leo ni upi?