•Michael alisema ndoa yake ya miaka kumi ilivunjika mwaka wa 2022 wakati mkewe alipotoroka kwa madai ya fitina.
•Wakati Pranice alipopigiwa simu alishika ila hakuzungumza, jambo ambalo lilimshangaza sana mtangazaji Gidi
Michael Otieno,39, kutoka Eldoret alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Pranice Mudeva ambaye alitengana naye miaka miwili iliyopita.
Michael alisema ndoa yake ya miaka kumi ilivunjika mwaka wa 2022 wakati mkewe alipotoroka kwa madai ya fitina.
"Nilipata mke wangu akiwa na majirani. Alikuwa anasema ati kwa nyumba simpei chakula. Nilitoka kazi nikapata ameenda kurent nyumba yake. Nilienda huko tukaongea akarudi. Kurudi akakaa kidogo akaenda kwao," Michael alisimulia.
Aliongeza, "Kuna siku nilimpigia simu akakula. Mara anapatia mama mwingine ananidanganya ati ni mama yake nimtumie pesa. Nikamtumia pesa akakula. Sijawahi kuenda kwao. Tulikuwa tunapanga kuenda kwao ndio akatoroka."
Wakati Pranice alipopigiwa simu alishika ila hakuzungumza, jambo ambalo lilimshangaza sana mtangazaji Gidi
"Kuku anawika. Wewe umenyamaza. Inaweza kuwa ni network? Mbona tunaskia kuku akiwika huko nyuma. Pranice anataka kutumalizia credit," Gidi alisema.
Michael alisema, "Tuliongea na yeye hata juzi. Yeye anasema tu nimtumie fare. Saa hii vile maisha ni ngumu hivi, unatuma pesa tu inaenda free? Mtoto ako sawa hata anaenda shule. Kuna wakati amekuja hadi Eldoret akaniona lakini hakunisalimia. Alinipigia simu tu baadaye akaniambia ameniona."
Je, una maoni ama ushauri upi kuhusu Patanisho ya leo?