Patanisho:Jamaa aomba msamaha babu yake baada ya kuita nyanya yake mchawi

Eugene alikiri kuwa alikosana na babu yake tangu 2019 ,Mzee Joram Makovi, baada ya kuita bibi yake mchawi.

Muhtasari

•Eugene alikosana na babu wake tangu Novemba 2019 baada ya kumtusi bibi yake kuwa ni mchawi.

•Mzee Joram alikiri kuwa yeye hana makosa na mtu yoyote na kama Eugene anataka msamaha lazima aongee na mjomba wake  anayejulikana kama Fred.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Eugene Makovi,30 kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na babu wake bwana Joram Makovi mwenye umri wa miaka 78.

Eugene alisema kuwa alikosana na babu yake tangu Novemba 2019 baada ya kumwambia mzee huyo kuwa bibi yake ni mchawi na anataka kumuua. Eugene aliongeza kuwa amelelewa na babu yake tangu  utotoni pindi tu mama yake alipoaga dunia mwaka wa 2005.

"Babu yangu ambaye alizaa mama  aliamua kuoa mke ambaye angemtunza wakati wa uzeeni baada ya mimi kuondoka. Bibi Huyo alipokuja hatukuwa tunaelewana ,akaanza kupiga vita mke wangu, nikaamua kutoka kwa hiyo boma." Eugene  alisimulia.

Aliongeza kuwa  "Nilichukua harakati ya kutoka kwa hiyo boma, nikamtusi kuwa ni mchawi.Nilipokutana na babu aliniambia nisiwahi mpigia simu tena.Kutoka 2019,sijaongea na babu.Niko na familia Nairobi na nahitaji kuwa na mtu ambaye naweza zungumza naye kama mmoja wa familia yangu ambaye sasa ni babu yangu.Babu amenisomesha tangu 2005 tangu mama wangu aage dunia.

"Babu yangu alikuwa na wake wanne, yule ambaye alikuwa ananilea alikufa mwaka 2009 na tangu hapo nimekuwa bila nyanya.Nyanya mkubwa ako upande wa Malava.Tangu mwaka huo niliamua kuoa ,babu pia akaona ni heri atafute mtu wa kukaa naye kwa boma sababu mimi ningekuwa namaliza muda mwingi na bibi yangu.'

 Vile vile Eugene alisema: "Nilimuita bibi ya  babu yangu mchawi kwa sababu ilitokea kuna mtoto wa mjomba wangu aliaga dunia baada ya mimi kupigana na yeye.Sasa katika harakati hizo,nikatembea kwa maombi ikafahamika huyo mama ndiye alikuwa na hio mipango yote. Kutokana na hasira nilimpigia babu simu kuwa bibi yake ni mchawi.Nilipomuelezea babu hakutaka kuniskiza na tangu siku hio tukakosana."

Mzee Joram alipopigiwa simu alisema kuwa yeye hamjui Eugene na  hana makosa na mtu yoyote na hivyo kukata simu.

Alipopigiwa kwa mara ya pili mzee alisema: "Penye alikosea aende asamehewe huko,mimi sijajua hiyo"

Aidha mzee alipigiwa simu kwa mara ya tatu huku bibi yake mzee Joram akipokea simu. Eugene alijaribu kumwomba nyanya yake msamaha, Bibiye mzee alisema kuwa yeye hana  shida na Eugene.

"Mimi sina makosa na wewe,mzee ndiye ako na shida na wewe.Mzee anasema lazima upigie Fred simu {mjomba wake Eugene} ndiyo akusamehe." Bibiye mzee alisema.

Je,una maoni au shauri upi kuhusu patanisho ya leo?

Jamaa aita nyanya yake mchawi baada ya vita na