"Nimeua nani!" Mwanadada aliyemtema jamaa kwa kuchelewa kukutana naye ashtuka kupigiwa na Gidi

"Mimi simpendi. Huyo mtu niliona ata hatupelekani na yeye mahali. Hakuna kitu huwa ananipea," Nyambura alisema.

Muhtasari

•Vincent alisema mahusiano yake na Nyambura yaliharibika Jumapili baada ya yeye kuchelewa kufika mahali ambapo walikuwa wamekubaliana kukutana.

"Nilienda nikapata amesimama hapo kwa stage ya kwao, na zimejaa hapo. Alifanya hata nikose kuenda kanisa," Nyambura alisema.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Vincent Bett ,29, kutoka Ruiru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Margaret Nyambura ,29, ambaye alikosana naye wiki iliyopita.

Vincent alisema mahusiano yake na Bi Nyambura yaliharibika siku ya Jumapili baada ya yeye kuchelewa kufika mahali ambapo walikuwa wamekubaliana kukutana.

"Tulikuwa tuende mahali siku ya Jumapili alafu nikachelewa kiasi. Niliamka nikaanza kufua kiasi nikachelewa. Tulikuwa tumekubaliana kuenda saa nne mimi nikaenda saa tano. Baada ya hapo alikataa kuniongelesha na akaniweka blacklist," Vincenty alisema.

Aliendelea, "Huwa ananishuku ati labda nikichelewa nimeenda kwa mtu mwingine na ni uongo kabisa. Mimi sijawahi kufikiria kitu kama hiyo. Alikuwa amesema tupatane kabla ya saa nne.  Tulikuwa tumepanga kabla ya mwisho ya hii mwaka tuoane. Nilikuwa niende kwao mwezi wa nne. Anajulikana kwetu."

Alibainisha kwamba hana njia nyingine ya kumfikia mpenziwe kwani tayari amemblock na hajui rafikiye ata mmoja.

Bi Nyambura alipopigiwa simu mwanzoni alisikika kushangaa kwa nini alikuwa akipigiwa simu na Radio Jambo.

"Uui, Nimeua nani?" alishangaa.

Aliendelea kumlalamikia mpenzi huyo wake na kumtaja kama muongo mkubwa.

"Huyo ni muongo. Alinitoa kwa nyumba saa tatu akaniambia tutapatana. Mimi niliamka mapema nikajitayarisha nikaenda stage. Nilimpigia simu akaniambia ati hakuna magari. Nilikuwa naona magari zikienda na zikirudi. Nilipata amesimama hapo kwa stage ya kwao, na zimejaa hapo. Alifanya hata nikose kuenda kanisa. Hata alipatia rafiki yake anidanganye ati hakuna magari," alisema Nyambura.

Vincent aliendelea kusisitiza kwamba alikuwa anafua na ndiposa alichelewa.

"Kwani alikuwa anafulia kwa stage? Huwa unanidanganya hivyo. Mimi na wewe apana. Achana na mimi sasa. Mpaka unapatia Tonny anidanganye ati hakuna magari, na mko kwa stage.Nilisimama Ruiru saa moja. Alafu nikaenda kwa stage yao nikampata hapo. Ulikuwa unasimama tu hapo kwa stage, si ungesema tu tupatane siku nyingine!" Nyambura alilalamika.

Vincent alisema, "Hapo nilikosea. Hakuna kitu ingine nilikuwa nafanya.Nipee nafasi ya mwisho, sitarudia tena. Tumetoka na wewe mbali"

Nyambura aliendelea kulalamika na hata akaweka wazi kwamba hampendi Vincent.

"Mimi simpendi. Huyo mtu niliona ata hatupelekani na yeye mahali. Wewe ndo unamfikirianga tu, yeye hawezi.Hakuna kitu huwa ananipea. Nikihesabu naona haiingiani.Nimemsamehe lakini kurudiana ndio itakuwa ngumu. Ata marafiki huniambia huyo mtu apana, aendelee tu na maisha yake... " alisema.

Pia alitupilia mbali uwezekano wa kufunga ndoa na Vincent akisema, "Kuona na nani? Aone wazazi ajena ako na mtoto huko? Si kwanza alee mwenye ako na yeye."

Je, maoni yako ni yepi kuhusu Patanisho ya leo?