Patanisho: "Aah, apana!" Mwanadada ashtuka sana kuskia anatafutwa na Gidi na Ghost

Caleb alikubaliana na uamuzi wa mkewe wa kutengana ila akamwagiza amrudishie mtoto.

Muhtasari

•Caleb alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika Julai mwaka huu baada ya mkewe kushawishika na fitina za watu ambao walimharibia sifa.

•Gidi alipofanya jaribio lingine la kumtafuta Shalon, aliweka wazi kuwa hataki kabisa kurudiana na mzazi huyo mwenzake.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Caleb Malang' Muchika ,23, kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Shalon Njambi ,23, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Caleb alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika Julai mwaka huu baada ya mkewe kushawishika na fitina za watu ambao walimharibia sifa.

"Tulikaa na mke wangu kwa muda na hatukuwahi kukosana tangu tuanze kuishi na yeye. Kabla nihame, tulikuwa tunaishi na yeye tukawa tunakosana, shida ilikuwa ni yeye kusikia maneno ya watu eti niko na mipango ya kando. Nilijaribu kumwambia aache kusikia maneno ya watu lakini hataki kusikia," Caleb alisema.

Aliongeza, "Nimemuoa rasmi. Nimeenda kwao mara kadhaa kujitambulisha. Tukikosana huwa naenda kwao tunasuluhisha. Kuna wakati nilienda kuishi kwao Kirinyaga, nikawa naenda kazi Nairobi. Bado tulikosana."

Shalon alipopigiwa simu, mwanzoni alikataa kupatanishwa na kukata simu mara moja.

"Aah, apana!" Shalon alisema aliposikia anatafutwa na Gidi.

Gidi alipofanya jaribio lingine la kumtafuta Shalon, aliweka wazi kuwa hataki kabisa kurudiana na mzazi huyo mwenzake.

"Haiwezekani. Yeye ashughulike kivyake. Huyu Caleb ni mtu mzuri sana. Nimezaa naye lakini tabia zake ni mbovu. Nimejaribu kumwambia lakini habadiliki. Nimeamua tupeane muda kama tutarudiana lazima," alisema.

Aliongeza, "Kama mmekosana kwa nyumba, yeye ni vita tu. Wiki haiwezi isha kama hajakupiga. Wanawake. Vitu kidogo ashaambia wazazi. Mambo ya vita mimi sitaki, na miaka yangu bado ni ndogo bado."

Caleb alikubaliana na uamuzi wa mkewe wa kutengana ila akamwagiza amrudishie mtoto.

Shalon alimwambia, "Kama unataka mtoto umkujie nyumbani na mtu mmoja wenu. Sitakubali upeleke mtoto wangu kwa hao wasichana."

Je, ushauri wako ni upi kwa wawili hao?