Patanisho: Jamaa afumaniwa na mkewe mjamzito akiwa kitandani na mwanamke mwingine

Muhtasari

•Kiprop alikiri kuwa hakuwa anamtendea vyema mke wake katika kipindi ambacho walikuwa kwenye mahusiano.

•Kiprop aliahidi kuwajibikia mpenzi wake pamoja na mtoto wao huku akiahidi kuwa mwaminifu katika ndoa.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Ryan Kiprop alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Marion ambaye walikosana mwaka jana kufuatia mizozo ya kinyumbani.

Kiprop alikiri kuwa hakuwa anamtendea vyema mke wake katika kipindi ambacho walikuwa kwenye mahusiano.

Pia alikiri kuwa takriban miaka miwili iliyopita wakati Marion alikuwa amebeba ujauzito wa mtoto wao aliwahi kumfumania na mwanadada mwingine nyumbani kwao.

"Tulikuwa tumemaliza shughuli yetu akanipata. Hakuwa ameniambia anakuja, alinifumania  Wakati huo alikuwa mjamzito. Nilimuongelesha kidogo alafu nikamfungia kwa nyumba kisha nikazidikisha yule msichana huyo mwingine," Ryan alisimulia.

Alifichua kuwa alimpachika Marion ujauzito akiwa katika kidato cha pili na hivyo kukatiza masomo yake.

Kando na kuwa na kufumaniwa na mwanadada mwingine, Kiprop alikiri makosa yake mengine yakiwemo kutowajibikia mtoto, kulewa sana, kutoonyesha mpenziwe mapenzi na kumtendea madharau. 

"Huwa namkosea, nakunywa pombe, sisaidii mtoto, anapata jumbe za wasichana wengine kwa simu. Alikuja nyumbani desemba akapata meseji za wasichan kwa simu yangu. Mtoto wetu ana umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu," Alisema.

"Huwa tunaongea. Bado ako na machungu kutokana na tabia zangu.Wazazi wangu wanajua. Pia wazazi wake wanajua kuhusu mahusiano yetu,"

Kiprop hata hivyo alisema tayari amejuta matendo yake maovu na yupo tayari kubadili tabia zake.

Marion alipopigiwa simu alikubali kumsamehe Kiprop na kumsihi abadili mienendo yake. Marion alimhakikishia mpenzi wake kuhusu upendo wake mkubwa kwake. 

"Nakupenda pia. Uanze kushugulikia mtoto. Na uache kukunywa pombe," Marion alimwambia Kiprop.

Marion pia aliapa kurudi shuleni hivi karibuni.

Kiprop aliahidi kuwajibikia mpenzi wake pamoja na mtoto wao huku akiahidi kuwa mwaminifu katika ndoa.

"Nitakuwa namshughulikia mtoto. Nitamuoa Marion. Nitakuwepo katika maisha yake. Marion nakupenda sana. Sitawahi kuchezea sana. Sitakuwa nakukosea tena," Alisema.