Patanisho: Mipango ya ndoa yakwama baada ya wapenzi kubadilishana simu, wanaume kupiga simu ya mwanadada

Simon alidai kwamba wanaume wengi walikuwa wakipiga simu ya mkewe.

Muhtasari

•Simon alisema mahusiano yake na Mercy ya miaka minne yalikumbwa na hitilafu mwezi Septemba baada ya wao kubadilishana simu.

•Mercy alipopigiwa simu, mwanzoni alidai kwamba hamfahamu Simon.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Simon Bahati ,22, kutoka Makueni alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Mercy Mwongeli ambaye alitengana naye mwaka jana.

Simon alisema mahusiano yake na Mercy ya miaka minne yalikumbwa na hitilafu mwezi Septemba baada ya wao kubadilishana simu.

"Siku moja alikuja akaniambia tubadilishane simu. Nilikubali. Baada ya kumpatia alikaa na simu yangu kwa wiki moja na mimi nikakaa na yake wiki moja," alisimulia.

Alidai kwamba wanaume wengi walikuwa wakipiga simu ya mkewe katika kipindi cha wiki moja ambacho alikaa nayo.

"Niliona majamaa wengi wakimpigia simu na kumchat. Nilipata amesave namba za wanaume kwa majina ya wanawake. Walikuwa wananiuliza ako wapi Mercy. Nilipomuuliza aliniambia ni machali wake," alisema.

Simon alisema mpenziwe alikasirika na kumtema baada ya kumwambia kuwa hakufurahishwa na jinsi wanaume wengi walikuwa wakipiga simu yake.

Mercy alipopigiwa simu, mwanzoni alidai kwamba hamfahamu Simon.

"Ni kama amewadanganya. Sitaki mastori mingi. Mimi ni mwanafunzi," alisema.

Mercy pia alibainisha kuwa hakuna kitu chochote ambacho alikuwa amepanga na jamaa huyo

"Tulikuwa tumepanga. Mbona wakati huo hakusema ni mwanafunzi," Simon alihoji.

Mwanadada huyo aliweka wazi kuwa ana miaka 19 na kwa sasa anaangazia masomo yake ya chuo kikuu.

Gidi alimwagiza Simon awache kulazimisha mapenzi kwa wasichana wadogo wa shule na badala yake atafute mwanake mwingine.

"Wacha amalize masomo. Tafuta mwanake mwingine,"

Mercy alisema, "Mimi simtaki na hatuwezi kusaidiana.Ata simjui poa!"

Simon hakuwa na lingine ila kukubali kuwa Mercy amefanya maamuzi yake tayari na hakuna uwezekano wa wao kurudiana.