Patanisho: Jamaa aachwa baada ya kufichulia mkewe kuwa ana mtoto nje ya ndoa

Kituma alikiri kuwa alimuoa Bosibori akiwa na miaka 16 na baadae akampeleka shuleni.

Muhtasari

•Kituma alisema kuwa mkewe aligura ndoa yao ya miaka saba mwezi uliopita baada ya kumshuku kuwa anatoka nje ya ndoa.

•Bosibori alikubali ombi la msamaha la mumewe na kumuambia amtumie  nauli ya kurudi siku ya Jumamosi.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama William Kituma (27)  alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake  Faith Bosibori (23).

Kituma alisema kuwa mkewe aligura ndoa yao ya miaka saba mwezi uliopita baada ya kumshuku kuwa anatoka nje ya ndoa. Alikiri kuwa alimuoa Bosibori akiwa na miaka 16 na baadae akampeleka shuleni.

"Alikuwa ananishuku mara mingi. Siku moja alichukua simu yangu akapata namba ya mpenzi wangu wa zamani. Alimpigia simu wakaletana juu alafu akatoroka," Kituma alisema.

Alisema kuwa mkewe tayari ameblock namba zake na hataki kuwasiliana naye licha ya juhudi zote alizofanya kumfikia.

"Namwambia apatie mtoto simu anakataa," alisema.

Kituma alimshtumu mpenziwe wa zamani kwa kuvunja mahusiano yake. Alikiri kuwa na mtoto mmoja na mwanadada huyo. 

"Kuna vile ex wangu anataka niachane na huyu. Niliona anataka kuniharibia ndoa. Hata nilifuta namba yake kwa simu yangu," alisema.

Bosibori alipopigiwa simu alithibitisha makosa ya mumewe na kueleza sababu zake kumtema na kurudi kwao.

"Kuna mwanamke alikuwa amezaa na yeye. Hakuniambia kabla anioe. Alikuja kuniambia wakati amenioa na tushazaa naye,"alisema.

Aliongeza "Mwanamke huyo alikuwa anampigia simu usiku na hata anatoka nje usiku. Baadae alikuja kuniambia wana mtoto pamoja alafu mimi nikatoka nikaenda kwetu,"

Kituma alimuomba mkewe kurudi nyumbani na kuahidi kubadili mienendo yake na kuwa mwaminifu katika ndoa yao.

"Hata hatuongei na yeye (ex) sasa "

Bosibori alikubali ombi la msamaha la mumewe na kumuambia amtumie  nauli ya kurudi siku ya Jumamosi.

"Bado nakupenda. Nitarudi tuendelee na ndoa yetu," Bosibori alimwambia mumewe.