Nilienda Mombasa na kuanza kazi ya Uganga,'Jamaa awatobolea marafiki zake siri

Muhtasari
  • Jamaa awatobolea marafiki zake jinsi alivyokuwa mganga baada ya kidato cha 4
Mbusi na Lion

Kuku wakiwa wengi wanamwaya mtama katika kitengo cha toboa siri, huku siri zao zikiwashinda kueka wanatoboa.

Jamaa mmoja alieleza jinsi alijiunga na kazi ya uganga, baada ya kuenda mjini Mombasa.

"Nilimaliza kidato cha nne mwaka wa 2015, rafiki yangu aliniita Mombasa ili tukatafute kazi, nilipofika hapo nilipatana na mganga na kunifunza kazi ya uganga

Baada ya muda tulikosana baada ya kuwachukua wateja wake, nilirudi nyumbani na kuanza kazi hiyo," Alieleza Jamaa huyo.

Je siri ya jamaa huyo iko wapi?

"Nataka kuwatobolea marafiki zangu ambao walinitembelea juzi kwangu na kunipata nikipea bidhaa za uganga uji, nataka niwaambie kwamba mimi ni mganga na kwamba siku nyingine wakija kwangu lazima wainie na mgongo, na kwamba wakipata chura na bidhaa zingine wasishtuke."