Nimeolewa na mama wa 'harrier' baada ya kumuomba 'lift'-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Jumatatu mwanamume mmoja alimwaya mtama jinsi alipewa 'lift' na mama kisha akamuoa
Mbusi na Lion

Kuku wakiwa wengi humwaya mtama kwenye kitengo cha toboa siri hata wakishindwa kuziweka moyoni wanazitoboa.

Katika kitengo cha toboa siri siku ya Jumatatu mwanamume mmoja alimwaya mtama jinsi alipewa 'lift' na mama kisha akamuoa.

KUlingana na mwanamume huyo, alikuwa anaishi Kayole, ambapo alimdanganya rafiki yake ameenda Mombasa ilhali yuko Nairobi.

"Nilipewa lift na mama wa harrier mwaka jana nilipokuwa nimetoka kutafuta kazi, baada ya hapo alinipelekea kwake na kisha akanioa

Nilimdanganya rafiki yangu kwamba naenda MOmbasa ilhali niko Nairobi, pia nataka kuwatobolea wazazi wangu siri niwaambie kwama nimeolewa na niko salama, na ng'ombe niliowanunulia mnilipewa hizo pesa na mwanamke huyo na hivi karibuni tutakuja nyumbani

Mama huyo ni datari,alinipeleka shule kujifunza jinsi ya kuendesha gari na niko sawa," Alisimulia mwanamume huyo.