Nilimnyakua mume wa rafiki yangu alipokuwa mgonjwa-Mwanadada amtobolea rafikiye siri

Muhtasari
  • Hawakukosea waliposema kikulacho ki nguoni mwako, kwani huyajui yalle rafiki wako wa karibu wamekupangia maishani mwako

Hawakukosea waliposema kikulacho ki nguoni mwako, kwani huyajui yalle rafiki wako wa karibu wamekupangia maishani mwako.

Kutokana na maarifa yangu kama uko kwenye mapenzi husidhubutu kumtambulisha mpenzi wako kwa rafiki yako ambaye una shauku naye kwamba anaweza kumnyakua.

Katika kitengo cha toboa siri mwanamke mmoja alimtobolea rafiki yake jinsi alimnyakua mpenzi wa rafiki yake.

Kulingana na mwanamke huyo alimnyakua kwa ajili yuko sawa, na wakati huo rafikiye alikuwa mgonjwa

Hii hapa siri yake;

"Nataka kumtobolea rafiki yangu siri kwamba nilinyakua mpenzi wake Freddie alipokuwa mgonjwa

Nilimnyakuwa kwa sababu yuko sawa," Alitoboa mwanadada huyo.

Sio mmoja au wawili ali tumeshuhudia wanandoa na wapenzi wakiachana kwa sababu ya marafiki, huku ugomvi kati yao ukinoga kila kuchao.

Kwa wanaume Je umewahi nyakuliwa na rafiki ya mpenzi wako au kuonyesha hisia kwamba anakutaka?

Kwa wanawake umewahi nyakua mpenzi wa rafiki yako au mpenzi wako amewahi nyakuliwa na ulihisi vipi?