Afueni kwa wapenzi wa soka! Angela merkel aruhusu Bundesliga kurejelea hali yake ya kawaida

28019540-8287775-image-a-24_1588666123420
28019540-8287775-image-a-24_1588666123420
NA NICKSON TOSI

Ligu kuu ya Ujerumani  Bundesliga sasa itaanza rasmi baada ya serikali kuitikia wito huo. Ligi hiyo sasa itaanza rasmi Mei 15 baada ya Angela Merkel kuruhusu michuano iliyokuwa imesalia kuendelea .

Kwa mujibu wa Reuters, Merkel amesema ligi hiyo itarejelea hali yake ya kawaida japo kwa kufuata masharti yaliyowekwa na serikali ili kudhibiti virusi vya Corona.

Vile vile serikali ya Ujerumani inapania kufungua maduka na maeneo mengine katika mkutano wao wa mwisho wa Mei 11.

Yamkini ligi zote ulimwenguni zilikuwa zimesitishwa kutokana na janga kuu la Corona .

Ligi kama vile ya Uingereza pia inapania kurejelea viwango vyake vya kawaida mapema mwezi huu ama ujao