Mashabiki wa Arsenal waliovalia jezi za Mkhitaryan wasimamishwa mjini Baku

mkhitaryan
mkhitaryan

Polisi mjini Baku wamenaswa kwenye video wakiwasimamisha mashabiki wa   waliokuwa wamevalia jezi ziliozandikwa jina la mchezaji Henrikh Mkhitaryan.

Nyota huyo wa Armenia alikataa kusafiri na kikosi cha Arsenal kwenda Azerbaijan kwa fainali ya leo usiku kuania taji la  akihofia usalama wake.

Mkhitaryan alikuwa amehakikishiwa usalama wake na UEFA na shirikisho la soka la Azerbaijani, hata hivyo picha zimechipuka zikionyesha mashabiki wa Gunners wakisimamishwa kwa kuvalia tu Jezi zenye jina lake.

Video iliyochukuliwa na  na kuwekwa kwenye Twitter, yaonyesha mashabiki wa Arsenal wakisimamishwa na polisi, wanaozuia safari yao kwa muda.

Anasubiri maagizo zaidi na kisha kuruhusu mashabiki hao kuendelea na safari yao bila bughudha.

The Gunners walihamakishwa na hatua ya mmoja wa wachezaji wao kutoweza kushiriki mchuano wenye hadhi ya juu kwao msimu huu.

Mkhitaryan ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Armenia, nchi ambayo imejipata katika mzozo mkali wa mipaka na Azerbaijan huku pande zote zikipigania kutwaa eneo la Nagorno-Karabakh.

Meneja mkurugenzi wa Arsenal Vinai Venkatesham aliambia jarida la the Financial Times Business of Football summit wiki iliyopita: 'Napata ugumu kueleza vile nahisi. Twahisi hali hii haukubaliki.

Wachezaji wa Gunners walikuwa wamepanga kuvalia jezi zenye jina la Mkhitaryan wakati wa kupasha misuli moto kabla ya fainali, kama  , wamekatazwa kufanya hivyo kuambatana na kanuni kali za UEFA.

Lakini wachezaji wamesisitiza kwamba watafanya kila juhudi kushinda kombe hilo kwa heshima ya mchezaji mwenzao.

'Bila shaka tumevunjwa nyoyo na kutokuwepo kwake hapa lakini nafikiri tulizungumza sana kuhusu Mkhitaryan, na maswala mengine ya kisiasa, na sasa ni wakati tuzungumziye kandanda,' alisema Xhaka.

'Bi nguzo sana kwetu, na tunataka kumpa kombe kesho.'

-Dailymail