Arsenal yamfuta kocha Unai Emery, sababu zatolewa

unai
unai

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amefutwa kazi baada ya kuongoza timu hiyo kwa kipindi cha miezi 18.

Akizungumza kwa niaba ya bodi ya Arsenal, Josh Kroenke alisema,

"Tunamshukuru sana Unai na kocha wenzake ambao walitia bidii katika juhudi zao za kurudisha kilabu kushindana kwa kiwango ambacho sisi tunatarajia na kudai. Tunamtakia Unai na timu yake mafanikio katika siku zake za usoni. "
 
Klabu hiyo ilitangaza kuwa aliyekuwa naibu wa Unai Emery na mchezaji wa zamani wa Arsenal, Freddie Ljungberg ndiye atakayechukua hatamu ya klabu hiyo hadi watakapo teua kocha mwingine.
Tumemuuliza Freddie Ljungberg kuchukua jukumu la timu ya kwanza kama kocha mshikilizi. Tuna imani kamili kuwa Freddie atatupeleka mbele.