Bajeti iliyosomwa inamtoza mwananchi uchumi wa juu - Gavana Mutua

Gavana wa Machakos Alfred Mutua amaetoa wito kwa baraza la kiuchumi la taifa kutoa matarajio ya uchumi wa kenya katika siku za usoni kutokana na hali ya kiuchumi inayoshuhudiwa kwa sasa.

Mutua anasema bajeti iliyosomwa hivi majuzi inamtoza mwananchi uchumi wa juu bila ya mpango wowote wa kutoa nafasi za kazi kwa wananchi.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge sasa wanataka waziri wa fedha kubuni mbinu ya kuwapa wahudumu wa bodaboda bima ya gharama ya chini kuliko iliyopendekezwa katika bajeti.

Mbunge wa ikolomani Benard Shinali na mwakilishi wa akina mama kaunti ya kakamega Elsie Muhanda wamesema kuweka gharama ya juu kwa wanabodaboda kutagandamiza sekta hiyo ambayo imebuni nafasi za kazi kwa wanabodaboda wengi.