che;

Bamba Sport kupeperusha mechi dhidi ya Chelsea na West Ham

Baada ya wiki nyingine iliyojaa kilio na vishindo katika ligi ya mabingwa wa bara Uropa na pia Europa, wikendi imewadia na kama kawaida, ligi kuu ya Uingereza imetuandalia mechi baab kubwa.

Mwanzo, wewe kama shabiki mkuu wa ligi kuu ya Uingereza, unapaswa kujua kuwa runinga nambari moja, Bamba sport itakuwa ikikupeperushia mechi ya Chelsea dhidi ya West Ham.

Mechi hii ijulikanayo kama ‘London derby’ itapeperushwa moja kwa moja jumamosi hii kuanzia mida ya 5:30 jioni.

Mahasimu hawa wa mtaa wa London wamemenyana miaka nenda miaka rudi ila, Chelsea ndio walio na wingi wa ushindi huku mara ya mwisho West Ham kuwanyuka ‘The Blues’ ugani Stamford Bridge ikiwa Septemba, 2002.

Vijana wa Frank Lampard wamekuwa wakiandikisha matokeo mazuri ambayo imepelekea wao kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye jedwali la EPL.

Hata hivyo, Jumatano walilazimika kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Valencia ugani Estadio Mestalla katika michuano ya kuwania ubingwa barani Ulaya.

The Hammers nao wamejipata kwenye hali tatanishi huku kocha mkuu Manuel Pellegrini akijipata kwenye tishio la kupoteza kazi yake.

Kwa sasa, West Ham wanashikilia nafasi ya 17 baada ya kupotea mechi yao 3-0 dhidi ya Burnley.

Mechi zingine za kutazamiwa wikendi hii ni;

Newcastle vs Man City

Norwich vs Arsenal

Man United vs Aston Villa

Liverpool vs Brighton

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments