Kuna wakati nilikuwa side-chic kwa miaka-Diana Marua afichua

Muhtasari
  • Kuna wakati nilikuwa side chic wa mwanamume aliyekuwa na familia
  • Niliwapenda wanaume kwa ajili ya pesa, nilikuwa na mwanamume wa kulipa kodi ya nyumba, kununua nguo na kadhalika
Diana 1
Diana 1

Diana Marua mkewe msanii Kevin Bahati, ameweza kufichua siri zake za ndani huku akithibitisha hamna mtu ambaye ni kamili na hatupaswi kuwaukumu wenzetu bila ya kujua hali yao.

Mama huyo alifichua kuwa alikuwa anashtuka sana alipokuwa anawaona mashabiki wakitoa maoni kuwa alimpenda Bahati kwa sababu ya mali yake na kwa sababu ni tajiri.

Pia alifchua kuwa alipokuwa mpenziye Bahati alikuwa anapatana naye huku akitumia aina tofauti za gari huku akidanganya Bahati kuwa ni za kukomboa.

Huku akizungumza kupitia kwenye mitandao ya youtube, Diana alisema kuwa alikuwa anawachumbia na kuwapenda wanaume kwa ajili ya pesa zao, na alikuwa anazipata kwa urahisi, huku akitumia pesa hizo kununua nguo viatu na kuwekeza.

"Nakumbuka kuna wakati nilikuwa side chic kwa mwanamume ambaye alikuwa na familia, nilimpenda sana mwanamume huyo nilikuwa na mtu kulipa kodi ya nyumba, wa kununua nguo kunipeleka kujivinjari

nilikuwa nashtuka watu wakisema kuwa nampenda Baha kwa ajili ya pesa." Alieleza Diana.

Pia alisema kuwa kuna wakati alijihisi mpweke licha ya pesa ambazo alikuwa anapokea na kumuomba Mungu ampe mume wake.

Alisema kuwa alikuwa na marafiki ambao walimsahauri aweze kuendelea na uhusiano wake, hii hapa video yake;

#mytestimony #ThankyouLord