Wanandoa mashuhuri wenye mitindo bora zaidi mwaka wa 2020

Muhtasari
  • Tazama wanandoa mashuhuri ambao wanamitindo bora zaidi ya mavazi 2020
lulu 2
lulu 2

Wengi wao tumewaona kwenye hafla tofauti wakiwa wamehudhuria na wake zao huku wakiwapendeza wengi kwa ajili ya mitindo yao ya mavazi.

Katika makala haya tunaangazia, wanamuziki,waigizaji,wachekeshaji na watu wengine ambao wamenoga katika sekta ya mitindo ya mavazi mwaka huu wa 2020.

Wengi wanasema kwamba mwaka wa 20202 haujakuwa mwema kwao baada ya janga la corona kuingia nchini huku mambo mengi yakipigwa marufuku na masharti mengi kuwekwa.

Lakini watu wengi mashuhuri hawajawacha kuwapendeza mashabiki wao kwa ajili ya mitindo yao bora ya mavazi.

Hii hapa orodha ya wanandoa mashuhuri wenye mitindo bora zaidi 2020;

1.Nameless na Wahu

Wanandoa hao wawili ni wakupigiwa mfano na watu wengi, baada ya kuwaonyesha mfano wa ndoa na hata kuwa katika orodha ya watu wenye mtindo bora zaidi katika mavazi yao.

2.Wajesus

Wanandoa hao wamekuwa mara kwa mara wakipakia picha za mavazi yenye mitindo mipya na kupendwa na wengi.

3. Bahati na Diana Marua

 

Wawili hao awali wamekuwa wakipakia picha wakiwa wamevalia mavazi yamefanana na yenye mitindo bora zaidi mwaka wa 2020.

4.Rashid abdalla na Lulu Hassan

Wanahabari hawa mara kwa mara wmekuwa wakiwaacha mashabiki wao na maswali nani aliunda nguo zao kwa maana ni za kipekee.

lulu 3
lulu 3

5.Alfred Mutua na Lilian Ng'ang'a

Gavana huyo wa kaunti ya Machakos na mkewe pia hawajaachwa nyuma katika orodha hii kwa maana wamekuwa wakivalia mavazi yenye mitindo bora zaidi mwaka huu wa 2020.