Eric Omondi amwanika Ringtone kwa kummenyelea mmoja wa wake zake

Muhtasari
  • Eric Omondi amwanika Ringtone kwa kummenyelea mmoja wa wake zake
  • Hii ni baada ya mwanamke huyo kufahamisha Eric kinachoendelea

Kipindi chake Eric Omondi cha 'Wife Material' kilipata watazamaji wengi,huku kupiga kura kukitarajiwa kuanza jumatano wiki hii.

Eric anataka kusaidiwa kumchagua mke wake, na ambaye wanamitandao wanaona anafaa kuwa mke mwema kwa mchekeshaji uyo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Eric amemuanika msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko kwa kumnyemelea mmoja wa wake zake.

 

Apoko alimwalika Mwikali nyumbani mwake Runda, ambapo alihisi kuwa hana nia nzuri kwa maana alimhahidikumpa shillingi 100,000.

Eric alimuonya Ringtone na kumwambia awachane na wake wake.

"HAPPENING NOW!!! @ringtoneapoko has lured one of my wives to his place🤦‍♂️🤦‍♂️🤦‍♂️🤦‍♂️ AMBIENI HUYU POKO AWACHANE NA MABIBI ZANGU." Aliandika Eric Omondi.