Vera ajibu madai ya kutowahi kumpenda ex wake Brown Mauzo, azungumzia kurudiana naye

Madai yaliibuliwa kwamba alikuwa na Mauzo kwa sababu tu alitaka kupata watoto wenye sura nzuri.

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto wawili alilazimika kujibu madai kwamba hakuwahi kumpenda mwimbaji huyo mzaliwa wa Pwani.

•Katika majibu yake, Vera aliweka wazi kuwa hakuna nafasi ya kurudiana na baba wa watoto wake wawili.

walithibitisha kutengana Agosti 2023.
Vera Sidika na Brown Mauzo walithibitisha kutengana Agosti 2023.
Image: HISANI

Mwanasosholaiti mashuhuri wa Kenya Vera Sidika amefunguka kuhusu uhusiano wake uliovunjika na mwanamuziki Fredrick Mutinda almaarufu Brown Mauzo.

Wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu na mashabiki wake kwenye Instagram siku ya Alhamisi asubuhi, mama huyo wa watoto wawili alilazimika kujibu madai kwamba hakuwahi kumpenda mwimbaji huyo mzaliwa wa Pwani.

Mwanamtandao mmoja aliibua madai kuwa sosholaiti huyo mrembo alikuwa na Mauzo kwa sababu tu alitaka kupata watoto wenye sura nzuri.

"Usikasirike na hii, lakini ni kweli haukuwahi kumpenda mume wako. Ulikuwa unatafuta jeni nzuri (watoto),” mwanamtandao mmoja alimwandikia.

Vera hata hivyo alionekana kukanusha madai hayo akisema, “Lmaooo,Kama ni jeni nzuri hadi benki ya mbegu za kiume iko nayo. Kwa kweli unaweza hata kuchagua rangi ya macho unayotaka mtoto wako awe nayo.”

Mwanamtandao mwingine alimtaka mama huyo wa watoto wawili kufichua sababu halisi iliyomfanya aachane na mumewe wa zamani.

Alijibu, "Utalazimika kutazama Real Housewives Sn2 ili kujua."

Bado shabiki mwingine alitaka kujua kama amewahi kufikiria kutatua matatizo yake na mzazi mwenzake na kurudiana naye.

"Umewahi kufikiria, labda tu mngerekebisha mambo na kurudi pamoja kwa heshima?" shabiki aliuliza.

Katika majibu yake, Vera aliweka wazi kuwa hakuna nafasi ya kurudiana na baba wa watoto wake wawili.

“Oh babe hilo halitatokea kamwe. Kwa heshima,” alisema.

Mwishoni mwa Agosti mwaka jana, Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Alishukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"