Maceleb ambao hawakumaliza shule kwa ajili ya sababu moja au nyingine

Muhtasari
  • Maceleb ambao hawakumaliza shule kwa ajili ya sababu moja au nyingine
huddah (1)
huddah (1)

Si watu wote ambao wanafahamika sana na mashabiki na hata kujulikana nchini kote ambao walihitimu masomo yao.

Kuna maceleb ambao hawakumaliza shule kwa sababu moja au ingine.

Wengi wamepeana hadithi yao ya maisha na hata kukashifiwa na kukejeliwa na mashabiki na wanamitandao lakini hawakukata tamaa kwa maana walijua kuwa lazima watimize ndoto zao.

Hawa hapa maceleb ambao hawakumaliza shule;

1.Masauti

Msanii huyo wa bongo alifahamika sana kwa ajili ya kibao chake cha 'sokote'huku akipendwa na watu wengi kwa ajili ya mtindo wake wa kutoa vibao vipya.

Masauti akiwa kwenye mahojiano na radiojambo alisema kwamba hakuitimu kidato cha nne kwa maana wazazi wake walikuwa na shida ya kifedha huku akiwaondokea ndugu zake waweze kupata elimu.

2.DJ Shiti

Shiti ni mchekeshaji na pia muigizaji ambaye kwa sasa anafurahia  matunda ya bidii yake ya kazi yake licha ya kuwa hakukamilisha masomo yake.

3.Vera Sidika

Mwanasosgolaiti huyo hakukamilisha masomo ya chuo kikuu ili kusaka pesa na aweze kujikimu.

4.Huddah Monroe

Huddah pia hakumaliza shule katika chuo kikuu ili aweze kutafuta pesa.