Wakenya mashuhuri ambao wanapesa lakini wanafanya 'side hustles'

Muhtasari
  • Orodha ya watu mashuhuri ambao wanafanya side hustles licha ya wao kuwa na pesa

Kuna baadhi ya watu ambao waliamua kutotegemea mshahara au mapatao yao ya kila siku, na kuanza kufanya boashara ndogo.

Licha ya baadhi ya watu mashuhuri wa humu nchini kuwa na pesa na kuwa matajiri wa kupigiwa mfano waliamua hawatalaza damu bali watafanya 'Side hustle' ili kuendelea kutajirika.

Katika makala haya tutazingatia watu mashuhuri ambao wana biasha ra tofauti licha ya kuwa na pesa.

1.Betty Kyallo

Betty amekuwa mfano mwema kwa vijana haswa ambao wanasema kwamba hamna kazi, bali na Betty kuwa na pesa ana biashara ya kinyozi ambayo alizindua wiki jana na saluni ambayo kwa sasa inaendelea kufanya vyema.

Betty Kyalo
Betty Kyalo

2.Vera Sidika

Sidika ni mwanasosholaiti ambaye amekuwa kwenye mitandao ya kijamii mara kwa mara, bali na kuwa na pesa pia ana biashara ambayo inamletea pesa katika kaunti ya Mombasa.

3.Jalang'o

Jalang'o alifahamika san alipokuwa muigizaji katika kipindi cha papa shirandula, bali na kuwa mtangazaji ana biashara ya kuuza mayai na hata kuwa na chaneli yake ya mahojiano.

Jalang'o
Jalang'o

4.Akothee

Msanii huyo kwa hakika anafahamika sana kwa maisha yake ya kifahari, amekuwa akifanya biashara tofauti.

akoth stylish 1 (1)
akoth stylish 1 (1)