'Ni baraka kuwa nawe kama rafiki,'Ujumbe wake DP Ruto kwa Moses Kuria

Muhtasari
  • DP Ruto amwambia Moses Kuria haya siku hii yake maalum
  • Moses amekuwa mfuasi wake Ruto wa karibu na rafiki yake wa karibu

Huku mbunge wa Gatundu Moses Kuria akisheherekea siku yake ya kuzaliwa amepokea ujumbe wa kufana kutoka kwa naibu rais William Ruto.

Moses amekuwa mfuasi wake Ruto wa karibu na rafiki yake wa karibu.

Kupitia kwenye ujumbe wake Ruto wa siku hii maalum ya Moses Kuria alimwambia kuwa ni baraka tele kuwa naye kama rafiki.

 

Pia alimwambia kwamba ni mmoja wa mabingwa wa 'hustler nation'.

"Tunakusherehekea Mheshimiwa @HonMoses_Kuria unapofikisha miaka 50. Ni baraka kuwa na wewe kama rafiki na mmoja wa mabingwa wa harakati za hustler. Heri ya siku ya kuzaliwa!" Aliandika Ruto.

Mbunge huyo alimjibu naibu rais na kumwambia kwamba;

"Asante bosi wangu, nitabaki kuwa mwaminifu na sio msaliti kama wengine,"

Hizi hapa baadhi ya jumbe za wakenya baada ya ujumbe wake Ruto;

Francis Kauta: Happy New Year. It's cultic to follow your boss. You can be a good follower of Jesus Christ. If you can lose everything following a man who's going nowhere, how much successful will you be should you decide to follow Jesus?

Charles Tumbo: A true friend,thanks William for remaining a true friend to your buddies.for sir Kuria all the best as you enter the next stage helping the coming president in managing the national affairs.

 

Zeddy: We celebrate champions of democracy while others celebrate champions of hustlers....