'Asante kwa kuwa mvumilivu.' UJumbe wake muigizaji Kate Actress kwa mumewe huku akisherehekea siku ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Kate Actress amwamndikia mumewe ujumbe huu wakati wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa
  • Wawili hao walisheherekea miaka mitatu katika ndoa yao mwaka jana 2020
Kate-Actress-7
Kate-Actress-7

Noa ya muigizaji Catherine Kamau almaarufu Kate Actress na mumewe Phil Karanja ni ya kupigiwa mfano na wengi.

Wawili hao hawajaweza kuwa na drama kama baadhi ya watu mashuhuri ambao wamekuwa na drama kwenye mitandao ya kijamii kwa kutafuta kiki.

Phil akisheherekea siku yake ya kuzaliwa Kate alimshukuru kwa kuwa mvumilivu na kuwa kwenye maisha yake.

 

Kate alikiri kwamba wanampenda na mwenye mawaidha ya kusaidia kila mtu ambaye amekutana naye.

"Happy Birthday baba njeri, ikiwa uthabiti, na nidhamu alikuwa mtu. Asante kwa kuwa mvumilivu sana na asiye na ubinafsi

Wewe ni baraka kubwa sana kwetu, familia yako na kwa watu wengine wengi ambao umevuka njia. wewe ni kiongozi kama huyo

Mwerevu zaidi, lakini ndiye mtu mkimya zaidi kwenye chumba. Unatoa hekima kila wakati wa kulaani unapozungumza

Tunakupenda sana Karanja, Mungu akuhifadhi na akupendelee siku zote za maisha yako

Heri ya kuzaliwa mtu wangu, mr CEO, Baba k Squared, kamtu ka tahidi high, nk. 😂 wacha sasa nifulize my guy 😭," Aliandika Kate.