'Eric amekuwa akitia bidii kuwahimiza vijana,'Karen Nyamu amtetea Eric huku akikashifu kukamatwa kwake

Muhtasari
  • Mwanasiasa Karen Nyamu amtete Eric Omondi,mmwanasiasa huyo alisema mchekeshaji huyo amekuwa akitia bidii na hata kuvuka mipaka kuwahimiza vijana

Mchekeshaji Eric Omondi amekuwa akivuma kwa muda sasa baada ya kuzindua kipindi au shoo yake ya kwanza wa 'wife material'.

Siku chache zilizopita alianzisha kipindi cha pili cha Wife Material, huku akiingia kwenye shida, na kukamatwa.

Omodhi ameachili Ijumaa, Machi 12 kwa dhamana ya shillingi 50,000,hisia mseto zimetokea kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya watu wakimtetea na kumkukashifu Mchekeshaji huyo.

Mwanasiasa Karen Nyamu kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikashifu vikali kukamatwa kwake Omondi huku akisema amekuwa akitia bidii kuwahimiza vijana kutumia talanta yao kwa maana wengi hawana kazi.

"Kwa viwango vya juu vya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini, ubunifu hutegemea talanta, ubunifu, na mali miliki kama pembejeo kuu ya kupata na kuunda ajira kwa wasanii wenzao.

@ericomondi amekuwa akisukuma mipaka katika tasnia hiyo akihimiza vijana zaidi kutumia talanta yao na kupata riziki," Aliandika Karen Nyamu.

Aliongeza;

"Kwa hivyo ikiwa unahisi alisukuma sana na kipindi chake cha #wifematerial cha pili, kuna njia bora za kudhibiti yaliyomo

Kukamatwa na mashtaka ya wasanii sio njia ya kudhibiti tasnia ya filamu. Matokeo yake yanafikia mbali na ambayo hatuwezi kumudu kama nchi,"