Nilifikiria nitaomoka baada ya kipindi cha Eric Omondi-Manzi wa Kibera afunguka

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti Manzi wa kibera aweka mambo haya wazi
  • Huku aiongelelea kipindi hicho alisema kwamba licha yake ya kukejeliwa sana na mashbiki kwa aili ya kurudia nguo alijikubali jinsi alivyo

Mwanasosholaiti chipukizi anayefahamika kama Manzi wa KIbera alifunguka na kufichua kwamba alikuwa ameeka matumaini yake katika kipindi cha mchekeshaji Eric Omondi.

Pia alisema kwamba alifunga biashara yake ya kuuza nguo ili ampe Eric wakati wake wote.

"Bada ya kuambiwa kipindi kimeisha na hata si kusimama nilirudi nyumbani, pesa za shukrani ambazo ulipewa na Eric nimekula ziko karibu kuisha

 

Mwisho wa mwezi sijui nitampa mwenye nyumba nini, nilipatwa na msongo wa mawazo kwa sababu sina kazi ya kufanya 

Tulipokuwa katika 'Wife material' angalau nilikuwa napata chakula mara tatu kwa siku lakini mwisho wa siku nimerudi kibera sina pesa wala chakula

Nimekuwa nikikaa kwa nyumba nikiangalia runinga tu, kwa sababu watu wanaona kwa maana nafahamika sana lakini kw mfuko sina kitu," Alieleza Manzi wa kibera.

Huku aiongelelea kipindi hicho alisema kwamba licha yake ya kukejeliwa sana na mashbiki kwa aili ya kurudia nguo alijikubali jinsi alivyo.

"Kwanza nataka kumshukuru Eric kwa kunipa platform ya kujiendeleza,kwanza nilikuwa naamka na zimia na simama tena wanawake walikuwa na simu za nguvu na mimi na kasimu kangu tu nang'ang'ana nayo

mimi nilijikubali jinsi nilivyo, lakini najua siku moja nitaomoka ili nisirudie nguo kama vile nilikejeliwa kwa kurudia nguo moja katika kipindi hicho

Eric anajua kutunza watu, ni mara yangu ya kwanza kusimamiwa na mlinzi, mimi baada ya shoo hamna mtu alikuwa ananipigia simu ananiambia baada ya shoo niletee nguo zangu hizo zilikuwa zangu 

 

Nguo zile nilikuwa nauza ndio navaa sasa," 

Mwanasosholaiti huyo alisema kwamba yuko tayari kufanya kazi yeyote.