Gavana Alfred Mutua amsifu Rayvanny kwa kibao chake cha kumuomboleza Magufuli

Muhtasari
  • Gavana Alfred Mutua amsifu Rayvanny kwa kibao chake cha kumuomboleza Magufuli
  • Katika kibao hicho Rayvanny anauliza nani atakaye futa machozi ya watanzania, baada ya kifo chake Magufuli
alfred mutua
alfred mutua

Gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua siku ya Alhamisi kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter alimsifu msanii  wa bongo kutoka Tanzania Rayvanny kwa kutoa kibao cha kumuomboleza Magufuli.

Kulingana na Mutua licha ya kifo chake Magufuli kutangazwa, Rayvanny alitoa kibao baada ya saa chache huku akisifu kazi ambayo rais huyo alifanya alipokuwa mamlakani.

Katika kibao hicho Rayvanny anauliza nani atakaye futa machozi ya watanzania, baada ya kifo chake Magufuli.

 

PIa kinazungumzia jinsi watanzania wameachwa gizani, na majonzi huku mioyo yao ikilalama.

Mwaka jana huku Magufuli akifanya kampeni za uchaguzi mkuu, aliwaleta wasanii wa bongo pamoja huku akiunga mkono ndoto zao.

Asilimia kubwa ya wasanii hao walimpigia debe wakati huo, kifo chake Magufuli kilitangazwa na naibu wake Suluhu mnamo Jumatano Machi,17.

Mutua alisema kwamba Rayvanny alifanya jambo la haraka licha ya kutokuwa na wakati wa kutosha baada ya kutangazwa kwa kifo chake rais huyo wa jamhuri ya Tanzania.

"Wimbo wa ushuru na wa hisia kali "Kifo" kwa Rais Magufuli. Hilo lilikuwa jambo la haraka na kipande kilichofanywa vizuri

Wimbo huo ulitolewa takribani masaa 12 baada ya kutangazwa kwa kifo chake. Lazima nisikilize. Hapa kuna nusu ya wimbo. Pumzika kwa Amani Dk. J.P. Magufuli. #Magufuli 1/2." Aliandika Mutua.