'Upendo unaooneshwa kwenye Msiba wako haujawahi tokea,'Diamond azidi kumuomboleza Magufuli

Muhtasari
  • Diamond azidi kumuomboleza Magufuli, huku akisema upendo anaoonyesha hujai tokea
Diamond Platnumz

Huku watanzania wakizidi kumuomboleza hayati John Pombe Magufuli mbele ya mazishi yake yalioandaliwa ya Ijumaa wiki hii, baadhi ya wasanii wanaendelea kumuomboleza.

Wasanii mbali mbali Tanzania walitoa vibao ili kuonyesha ishara ya kumuomboleza mwendazake huku wengi wakimsifia kwa mengi aliyoyafanya kabla ya kukata roho na alipokuwa uongozini.

Magufuli alikuwa rais watano wa nchi ya Tanzania, ibada ya wafu ilifanyika maeneo tofauti, huku wananchi na wambolezaji wakiruhusiwa kuona mwili wake.

 
 

Diamond alikuwa rafikiye Magufuli, ambaye alisema kwamba alimsaidia kwa njia tofauti hasa alipokumbwa na shida yeyote.

Magufuli aliwasaidia sana wasanii wa nchi ya Tanzania huku akiwashika mkono katika sanaa yao.

Kupitia kwenye ukurasa wa instagram wake staa wa bongo Diamond Platnumz alisema upendo ambao unaonyeshwa Magufuli hajwahi tokea.

Pia alisema kwamba watu wanaonyesha jinsi walivyokuwa wanampenda wakati alipokuwa hai na mamlakani.

"Upendo unaooneshwa kwenye Msiba wako haujawahi tokea...na haya yote ni matokeo chanya ya Mema Uliyotufanyia....

Watanzania wanamjua nani ni mwema kwao, na leo hii imeidhihirishia Dunia kuwa ni Kias gani inakupenda....🙏🏼," Aliandika Diamond.

Mungu azidi kuilaza roho yake mahali pema peponi.