'Watu wanakupenda na kukuamini,'Ujumbe wake Diamond kwa Samia Suluhu

Muhtasari
  • Staa wa bongo Diamond Platnumz amempongeza raisi mpya wa jamuhuri ya Tanzania Samia Suluhu

Staa wa bongo Diamond Platnumz amempongeza raisi mpya wa jamuhuri ya Tanzania Samia Suluhu.

Samia aliapishwa kuwa rais wa Tanzania, mnamo Ijumaa, baada ya kifo chake John Pombe Magufuli.

Diamond alimtakia Samia kila lakheri anapoanza kazi yake na kuendeleza miradi ilioanzishwa ma Magufuli.

 

Suluhu alikuwa naibu rais kutoka mwaka wa 2015.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikuwa na haya ya kunakili.

"Hongera sana mama yetu SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuwa Raisi wa Kwanza Mwanamke Nchini Tanzania....Post na Comments za watu kuanzia mitandaoni Mpaka majumbani, zinadhihirisha ni kiasi gani watu Wanakupenda na WanaKuamini...nakutakia kila lakheri katika kuendeleza Mazuri aloyaanzisha Dr. John Pombe Magufuli na mengineyo mengi utayoyafanya 🙏🏼,' Aliandika Msanii huyo.

Wengine waliompongeza ni pamoja na Alikiba,Nandy, Queen Darleen miongoni mwa wasanii wengine.