“Wewe ni mtu mzuri na utaenda mbinguni” – Milly Chebby ammwambia mumewe Terence Creative

“Happy Birthday Babe @terencecreative. Wewe ni mtu mzuri na utaenda mbinguni ❤️❤️❤️ Tuma matakwa ya siku ya kuzaliwa kwa Mwenzi wangu,” Milly Chebby alimwandikia.

Muhtasari

• Akionekana kuwa na furaha, Terence Creative alijiandiia ujumbe maalum kwa kuongeza mwaka mwingine mmoja katika mzunguko wa maisha.

TERENCE na Mkewe
TERENCE na Mkewe
Image: FACEBOOK

Mchekeshaji maarufu wa Kenya, Terence Creative alisherehekea siku yake ya kuzaliwa wikendi iliyopita kwa njia maalum.

Akionekana kuwa na furaha, Terence Creative alijiandiia ujumbe maalum kwa kuongeza mwaka mwingine mmoja katika mzunguko wa maisha.

Mchkeshaji huyo ambaye amepiga marufuku watu dhidi ya kutumia maudhui yake kwenye insta stories zake aliweka wazi kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, ameweza kufanikisha vitu vingi, na ni jambo la kumshukuru Mungu.

“NAMSHUKURU MUNGU KWA MWAKA MWINGINE 🙏🎂🎂Mungu usipofanya jambo lingine umefanya zaidi ya kutosha, nisisahau hilo, nashukuru kwa yote uliyonipa, Asante kwa Neema, rehema na afya kwa kutaja tu lakini machache uliyofanya,” Terence alisema.

“Bwana endelea kunipa hekima ya kuthamini nilichonacho kila wakati nikitafuta nisichonacho, nikumbushe kila wakati kushiriki nilichopata sababu sikuwa nacho hapo awali, naomba usiwahi kuzoea miujiza yako midogo ambayo umefanya hapo awali, sasa na miaka ijayo. Nakushukuru Mungu kwa mwaka huu mpya na nyingi utakazonijalia sawasawa na mapenzi yako, zitumike kulitumikia kusudi lako, kukutukuza siku zote na kuathiri wengine, utukuzwe kila wakati katika hali zote,” alimaliza.

 Kwa upande wake, mkewe Milly Chebby alimsherehekea akimtaja kama mtu mzuri ambaye ataenda mbinguni moja kwa moja.

“Happy Birthday Babe @terencecreative. Wewe ni mtu mzuri na utaenda mbinguni ️ Tuma matakwa ya siku ya kuzaliwa kwa Mwenzi wangu,” Milly Chebby alimwandikia.