Akothee akasirika baada ya mama wa watoto 6 aliyempa makazi kuleta ex wake kuishi naye

Akothee alisema single mama huyo wa watoto 6 alimuomba msaada wa pahali pa kukaa baada ya mumewe kuharibu nyumba yao lakini baada ya kumpa msaada wa makazi, alichuua hatua ya kumleta mume huyo kwa hiyo nyumba.

Muhtasari

• “Ili kuzidisha hali hiyo, anamwalika mume wake wa zamani kukaa naye, na kusababisha usumbufu zaidi na hata kuwakosea heshima wafanyakazi wangu. " Akothee alisema.

Akothee
Akothee
Image: Facebook

Mjasiriamali Esther Akoth maarufu Akothee ameonesha kutofurahishwa kwake na hatua ya mama  mmoja aliyempa msaada wa makazi kuchukua hatua ya kumkaribisha aliyekuwa mume wake kuishi na yeye katika makazi mapya.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Akothee alisema kwamba anahisi kutumiwa vibaya kwani single mama huyo wa watoto 6 alimlilia kuwa mume wale ameharibu makazi yao na kumuomba msaada wa nyumba, ambapo alikwenda mbele na kumleta ex wake kwa hiyo nyumba ya msaada kutoka kwa Akothee.

“Inaonekana nimekuwa shabaha ya unyonyaji. Kwa ukarimu nimetoa makazi na rasilimali kwa mama asiye na mwenzi aliye na watoto sita, nikiwapa nyumba, ardhi kwa ajili ya kilimo, chakula, maji, umeme bila malipo, na elimu kwa watoto wake wote. Hata hivyo, pamoja na jitihada zangu, mwanamke huyu anaonyesha kutowajibika kwa watoto wake,” Akothee alisema.

Mjasiriamali huyo wa Akothee Safaris alifichua kwamba single mama huyo alimwambia mume wake ndiye aliharibu nyumba alimokuwa akiishi na wanawe, na hivyo kumtaka msaada wa makazi mbadala, lakini baadae akamleta tena huyo ex kwa nyumba hiyo ya msaada.

“Uvivu wake unadhihirika kwa vile anapuuza wajibu wake wa mzazi. Isitoshe, vitendo vya mume wake wa zamani, kubomoa makazi yake ya awali, vimemfanya kutafuta hifadhi katika boma langu bila ruhusa. Yeye huingia nyumbani kwangu kwa uhuru na kujisaidia kwa chochote anachotaka bila kujisumbua kuuliza.”

“Ili kuzidisha hali hiyo, anamwalika mume wake wa zamani kukaa naye, na kusababisha usumbufu zaidi na hata kuwakosea heshima wafanyakazi wangu. Hali hii imeniacha kuhoji hekima ya ukarimu wangu wa awali na kujiuliza jinsi nilivyoingia katika hali hiyo yenye matatizo,” alimaliza akisema kwamba tukio hilo limemuumiza sana.