Akothee afichua baby daddies wake huomba ushauri kwa mpenzi wake Nelly Oaks

Akothee amefunguka kuhusu uhusiano wa mpenzi wake Nelly Oaks na wazazi wenzake.

Muhtasari

•Alifichua kuwa mpenzi wake anafahamu uhusiano wake na baba za watoto wake na kwamba hata anashirikiana nao vyema.

•Aliendelea kumsifu mpenzi wake kwa ufahamu wake na kuzungumzia heshima aliyonayo kwa uhusiano wao.

na meneja wake Nelly Oaks.
Akothee na meneja wake Nelly Oaks.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee amefunguka kuhusu uhusiano wa mpenzi wake Nelly Oaks na wazazi wenzake.

Akothee alizungumzia suala hilo baada ya baadhi ya wanamitandao kuibua wasiwasi kuhusu jinsi Nelly Oaks, ambaye pia ni meneja wake anahisi kuhusu drama zake na wazazi wenzake.

Huku akiwajibu, alifichua kuwa mpenzi wake anafahamu uhusiano kati yake na baba za watoto wake na kwamba hata anashirikiana nao vyema.

“Usichukulie maisha yangu kwa uzito sana, cheka tu. Wacha maswali ya ooh wapi Nelly wapi Nelly. Nitawachanga muruke akili 🤣🤣🤣. Nelly anafahamu sana hali ya familia yangu anashirikiana vyema na baba za watoto wangu, kwa hakika nikiwa sielezeki wanafika kwake kwa ushauri,” Akothee alisema.

Mwanamuziki huyo aliendelea kumsifu mpenzi wake kwa ufahamu wake na kuzungumzia heshima aliyonayo kwa uhusiano wao.

"Wanajua ni yeye pekee ndiye anayeelewa lugha yangu 🤣🤣🤣,sasa tulia tukupange 🤣🤣🤣🤣🤣," alisema.

Aliongeza, “Sijawahi kuona mtu aliyekomaa kabisa kama Nelly maishani mwangu . Nilikwambia Nelly akinishika nadanganya atajua nimemtongoza huyo jamaa 🤣🤣🤣🤣.

Anajua jinsi ninavyompenda na jinsi ninavyomheshimu, mimi mwenyewe na uhusiano wetu. Endelea kusimama nami mpenzi. Akiani anyieuni ndege koso osiepna.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alitoa kauli hiyo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufoka kuhusu matukio yake ya hivi punde na mmoja wa wazazi wake mzungu.

Kwa muda mrefu, Akothee na Nelly Oaks wameaminika kuwa zaidi ya washirika wa kazi tu. Mara nyingi wamedokeza kuhusu kuwa wapenzi.

Takriban miezi minne iliyopita, mama huyo wa watoto watano alionekana kuthibitisha kufufuka kwa mahusiano yake na meneja wake wa muda mrefu Nelly Oaks katika kipindi cha moja kwa moja cha hivi majuzi kwenye mtandao wa TikTok.

Katika kipindi hicho ambacho alikuwa akiwahutubia mashabiki wake Nelly Oaks akimwandalia chakula maalum jikoni, Akothee alisikika akimwita meneja huyo wake ‘babe’ mara kadhaa, jina ambalo hutumika sana sana  wapenzi.

Nelly Oaks pia alisikika akimtaja Akothee kama mtu maalum kwake huku wawili hao wakishiriki matukio ya kimapenzi kwenye kamera.

“Hiki ni chakula cha jioni maalum kwa mtu maalum kama wewe. Ni surprise,” Nelly Oaks alisikika akimwambia mwanamuziki huyo.

Wakati wa kipindi hicho, Akothee alikataa ombi la nambari ya simu ya Nelly Oaks huku akifichua kwamba hata ana uwezo wa kufungua na kutumia simu yake.

“Kweli nikupatie namba ya Nelly? unadhani mimi nimetosheka? Mimi sijarudi soko, mimi ndiye soko, sigawani na mtu,” Akothee alisema.

Nelly Oaks pia aliweka wazi kuwa hapatikani kwa mwanamke mwingine