Niache nijibambe na mabesties kwa amani – Rue Baby aonya wanablogu na kudai yuko single

Rue Baby alisisitza kwamba siku atakuwa na mpenzi mashabiki zake watajua tu kwani hatoweza kumficha, lakini akasema kwa sasa wale vijana wa kiume anaoonekana nao si wapenzi wake bali ni mabesties tu wa kula raha pamoja

Muhtasari

• Itakumbukwa kwa muda mrefu, Rue Baby alikuwa akihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchekeshaji MCA Tricky baada ya wawili hao kuonekana pamoja katika sehemu mbalimbali.

 

RUE BABY
RUE BABY
Image: Instagram

Rue Baby, binti wa Akothee amethibitisha kwamba kwa sasa yuko single na hana mpenzi licha ya kuonekana sehemu mbalimbali akiwa na vijana wa kiume.

Kupitia video ambayo aliichapisha kwenye insta story yake, Rue Baby alisema kwamba ni wakati mzuri wa kunyoosha rekodi kabla wanablogu hawajakurupukia moja ya picha zake na marafiki zake wa kiume na kudai kuwa ni wapenzi.

Rue Baby alisema kuwa aliamua kutoa taarifa kuelezea hali yake kimahusiano, kwani hataki kuwaweka marafiki zake wa kiume katika wakati mgumu na wachumba wao wa kike, aisisitiza kuwa wao kwake ni ‘besties’ tu.

“Habari mashabiki wangu, kuna kitu nataka kuweka wazi kwa haraka mno. Ninataka kufurahia muda mzuri na marafiki zangu wa kiume kwa Amani. Nataka kuenda mitoko ya jioni na vilabuni na wao kwa Amani, ni marafiki zangu sawa,” Rue Baby alianza.

“Sitaki kuamka asubuhi nipate wanablogu wameeneza taarifa kwamba Rue Baby ako na mpenzi. Tafadhali, mnapofanya hivyo mnawaweka marafiki zangu wa kiume katika wakati mgumu na wapenzi wao. Ninataka kuweka wazi kwamba mimi kwa sasa siko katika mahusiano yoyote, angalau hatujafika hapo bado,” aliongeza.

Rue Baby alisisitza kwamba siku atakuwa na mpenzi mashabiki zake watajua tu kwani hatoweza kumficha, lakini akasema kwa sasa wale vijana wa kiume anaoonekana nao si wapenzi wake bali ni mabesties tu wa kula raha pamoja.

“Lakini wakati nitakuwa kwenye uhusiano mpya bila shaka nyinyi watu mtaona tu aidha vidole, ini, figo au kitu kingine chochote lakini kwa sasa nataka kufurahia na marafiki zangu wa kiume, ninataka kupost picha zao kwa Amani. Kila mtu ambaye mnapost huko nje wakati mnaniona naye, hao wote ni marafiki tu. Hakuna hata mmoja wao ambaye ni jamaa ningependa kuchumbiana naye,” alimaliza.

Itakumbukwa kwa muda mrefu, Rue Baby alikuwa akihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchekeshaji MCA Tricky baada ya wawili hao kuonekana pamoja katika sehemu mbalimbali.

Hata hivyo, Tricky alikuwa wa kwanza kuweka wazi kuwa hawakuwa wanachumbiana lakini wengi walipuuzilia mbali kauli zake wakimchukulia kwa mzaha kutokana na kwamba yeye ni mcheshi.